IQNA

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mwaka mpya ni Mwaka wa Uchumi wa Kimapambano, Uzalishaji na Ajira

22:06 - March 20, 2017
Habari ID: 3470902
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa kuanza mwaka mpya wa 1396 Hijria Shamsia akiwapongeza Wairani na Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa siku ya kuzaliwa Bibi Fatima Zahra SA na Sikukuu ya Nowruz na ameupa mwaka mpya jina la Mwaka wa Uchumi wa Kimapambano, Uzalishaji na Ajira.


Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, mwaka uliomalizika wa 1395 uliambatana na matamu na machangu kwa taifa la Iran. Ameashiria baadhi ya mafanikio ya taifa la Iran katika mwaka uliopita na kusema: Izza na heshima ya taifa la Iran ilishuhudiwa katika masuala mbalimbali ya mwaka uliopita na maadui duniani kote wamekiri na kutambua uwezo na adhama ya Iran.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, mahudhurio makubwa ya wananchi katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu (tarehe 10 Februari) wakijibu utovu wa heshima wa Rais wa Marekani na vilevile mkusanyiko mkubwa wa wananchi katika maadhimisho ya Siku ya Quds ni dhihirisho la utambulisho na malengo aali ya wananchi wa Iran. Ameongeza kuwa, wakatinchi jirani zinasumbuliwa na ukosefu wa amani, usalama na amani ya Iran katika mazingira yenye machafuko ya kikanda na kimataifa ni kigezo muhimu sana, na katika kipindi chote cha mwaka uliopita Wairani wamekuwa katika usalama na amani endelevu.

Ayatullah Khamenei amesema kwa msingi huo mwaka mpya wa 1396 anaupa jina la "Mwaka wa Uchumi wa Kimapambano (kimuqawama), Uzalishaji na Ajira" na kusisitiza kuwa, kuyafanyia kazi masuala hayo kutakuwa sababuya mafanikio na kwamba maafisa wa serikali wanapaswa kutoa ripoti ya matokeo ya utendaji wao kwa wananchi mwishoni mwa mwaka huu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia ametaja hima kubwa ya vijana na harakati pana za kiimani kuwa ni vigezo vingine vya mafanikio na maendeleo ya taifa la Iran katika mwaka uliopita na kusema: Kushuhudia harakati zenye nishati na ubunifu wa kielimu, kiutamaduni, kiuzalishaji na kimichezo za maelfu ya makundi ya vijana kote nchini Iran na kufanyika majlisina shughuli za kidini ni miongoni mwa masuala chanya na ya kufurahisha kwa nchi na taifa la Iran.

Ayatullah Khamenei ameashiria sisitizo lake la "hatua na vitendo" wakati alipoupa mwaka uliopita jina la "Uchumi wa Kimapambano, Hatua na Vitendo" na vilevile kazi nzuri zilizoripotiwa na viongozi wa serikali na kusema: Hata hivyo bado kuna masafa makubwa baina ya kazi zilizofanyika na matarajio ya wananchi na yeye mwenyewe, na kwamba tamwimu chanya na hasi zinapaswa kutathminiwa na kutazamwa kwa pamoja.

Amesema kuwa, kutilia maanani jina la "uchumi kimapambano" pekee hakutoshi, na kuhusunjia za utatuzi wa hali ya sasa amesema: Tiba ni kugawa uchumi wa kimapambano au ngangari katika nukta muhimu na kuu na kuelekeza jitihada zote za maafisa wa serikali na wananchi katika nukta hizo ambazo ni uzalishaji wa ndani na ajira hususan kwa tabaka la vijana.

3585319

captcha