IQNA

Misri kuasisi Baraza Kuu la Qur'ani

12:27 - July 06, 2017
Habari ID: 3471052
TEHRAN-(IQNA)-Waziri wa Waqfu Misri ametangaza kuundwa Baraza Kuu la Qur'ani nchini humo kwa lengo la kuimarisha viwango vya kuhifadhi Qur'ani na kuratibu vituo vya Qur'ani nchini humo.
Misri kuasisi Baraza Kuu la Qur'ani

Katika taarifa, Waziri wa Waqfu Misri Sheikh Mukhtar Gomaa ametoa agizo la kuasisiwa Baraza Kuu la Qur'ani Misri ambalo limetajwa kuwa na malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na: "Kustawisha kiwango cha kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu", "Kubuni Sera na Mpango Maalumu wa Kuimarisha Shule za Qur'ani", na "Kulinda Utamaduni wa Kiislamu katika Sekta ya Elimu".

Aidha baraza hilo litakuwa na majukumu mengine kama vile kuimarisha utafiti unaohusiana na qiraa ya Qur'ani Tukufu na kuhimiza harakati za Qur'ani kwa kuandaa mashindano ya Qur'ani.

Sheikh Gomaa ameongeza kuwa, mwenyekiti wa baraza hilo atakuwa ni waziri wa Waqfu huku likiwa na wanachama wasiopungua 7 na wasiozidi 15.

Misri ni mashuhuri duniani kwa wasomaji au quraa bora wa Qur'ani huku Waislamu wengi wakiwa wanavutiwa sana na Ustadh Abdul Basit Abdul Samad.

3615778

captcha