IQNA

PEW: Waislamu Marekani wanazidi kubaguliwa kutokana na sera za Trump

0:28 - July 27, 2017
Habari ID: 3471088
TEHRAN (IQNA) Uchunguzi umebaini kuwa, asilimia 74 ya Waislamu nchini Marekani wanapinga namna rais Donald Trump wa nchi hiyo anavyoamiliana vibaya na jamii ya Waislamu katika nchi hiyo.

Kituo cha Utafiti yaani Pew Research Center ( PEW) kimetangaza kuwa asilimia 74 ya Waislamu nchini Marekani wameutaja mwenendo wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo mkabala na jamii ya Waislamu nchini humo kuwa ni wa kiuhasama huku karibu asilimia 65 ya Waislami wakikosoa namna Rais huyo anavyoiongoza nchi hiyo.

Kituo hicho cha utafiti kimesisitiza kuwa mivutano imeongezeka katika uhusiano kati ya Rais Donald Trump na jamii ya Waislamu nchini Marekani kufuatia kupasishwa marufuku ya kuingia nchini humo raia wa nchi sita za Kiislamu. Matokeo ya utafiti uliofanywa na kituo hicho cha PEW yanaonyesha kuwa Waislamu nchini Marekani wanakabiliwa na ubaguzi mkubwa na kwamba Rais wa nchi hiyo amewaikasirisha na kuitia wasiwasi jamii hiyo ya Waislamu huko Marekani huku raia hao wakibainisha kutokuwa na imani narais huyo. Hii si mara ya kwanza kwa Waislamu nchini Marekani kutokuwa na imani na Rais kutoka chama cha Republican na kubainisha kutoridhishwa naye.

Waislamu nchini Marekani walikuwa miongoni mwa wakosoaji wa serikali hata wakati wa utawala wa George W. Bush, rais mstaafu wa nchi hiyo.

Pamoja na hayo, kuenezwa chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu kumepelekea idadi kubwa ya wasiokuwa Waislamu Marekani na nchi zingine duniani kupata hamu ya kuujua Uislamu ambapo wengi wanaopata taufiki hatimaye husilimu baada ya kuutambua ukweli. Taasisi ya PEW katika uchunguzi wake uliochapishwa Mei mwaka huu ilitangaza kuwa Uislamu ndio dini inayoenea kwa kasi zaidi duniani.

3463465

captcha