IQNA

Watu Milioni 15 Iran washiriki katika mpango wa kitaifa wa kusoma Qur'ani

12:49 - September 02, 2017
Habari ID: 3471152
Watu zaidi ya milioni 15 kote Iran wameshiriki katika mpango wa kitaifa wa kusoma Qur'ani Tukufu.

TEHRAN (IQNA)- Watu zaidi ya milioni 15 kote Iran wameshiriki katika mpango wa kitaifa wa kusoma Qur'ani Tukufu.

Mpango huo ujulikanao kama Bisharat 1451 ulimalizika Ijumaa ambapo ulijumuisha kusoma, kuhifadhi na kutafakari kuhusu Surah al Mulk na Surah Al Waqi'ah. Kwa mujibu wa katibu wa Mpango wa Bisharat 1451, Bw. Mohammad-Zadeh amesema mpango huo ulianza katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu. Sherehe za kufunga mpango huo zilifanyika Ijumaa katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini MA kusini mwa Tehran na kushirikisha idadi kubwa ya wasomaji na waliohifadhi Qur'ani Tukufu.

Amesema mpango wa Bisharat ulipewa nambara 1451 ikiashiria mwaka wa 1451 tokea kuteremshwa Qur'ani Tukufu.

Televisheni na radio za kitaifa pamoja na taasisi za serikali Iran zilishiriki katika kuandaa program hiyo ambayo iliandaliwa rasmi na Televisheni ya Qur'ani ya Iran.

Mohammad-Zadeh amesema kufnayika sherehe ya kufunga Bisharat 1451 katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini MA ni ishara ya kutangza tena utiifu kwa malengo matukufu ya muasisi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha amesema Bisharat 1451 ni kati ya harakati kubwa za Qur'ani nchini Iran huku akibainisha matumaini yake kuwa mpango wa mwaka ujao wa Bisharat 1452 utavutia watu wengi.


3636970
captcha