IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu na Ubaguzi, chanzo za kubakia nyuma vijana Waislamu Uingereza

23:29 - September 09, 2017
Habari ID: 3471164
TEHRAN (IQNA)-Uchunguzi mpya wa hivi karibuni unaonyesha kwamba, vijana Waislamu wanaoishi nchini Uingereza wamekuwa waathirika wakubwa wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi kuanzia shuleni, vyuo vikuu na hata maeneo ya kazi.

Tume ya Ustawi wa Kijamii nchini Uingereza Alkhamis ya Alhamisi imetoa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sheffield ambapo imeonya kwamba ni asilimia ndogo sana ya vijna wa Kiislamu ambao wanaweza kupata kazi ndani ya taifa hilo wakilinganishwa na vijana wenzao wa imani nyingine za kidini. Imefafanua kuwa, vijana hao wamekuwa wakinyimwa fursa za kuonyesha uwezo wao katika soko la kazi.

Uchunguzi huouliofanywa na Chuo Kikuu cha Sheffield umesisitiza kuwa, chuki dhidi ya Uislamu na ubaguzi wa kidini unaoshuhudiwa hii leo katika jamii ya Uingereza, ni kikwazo kikuu katika njia ya vijana Waislamu kufikia malengo yao. Aidha matokeo ya uchunguzi huo yanaonyesha kwamba, vijana wa Kiislamu ni wenye kufanya kazi kwa bidii, wapole na wenye matarajio ya kufikia malengo, huku akthari yao wakiwa wanaamini kuwa, kutokana na ubaguzi wa kidini uliokithiri, wanalazimika kufanya kazi mara 10 zaidi kuliko wenzao wasiokuwa Waislamu.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa Mwislamu mmoja kati ya watanao nchini Uingereza na eneo laWales, hufanya kazi kwa muda mrefu huku asilimia sita tu kati yao wakiwa ndio wanaofanikiwa kufikia daraja za juu za uongozi nchini humo. Kwa sasa Waislamu milioni tatu wanaishi nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa sensa ya hivi karibuni ya watu Uingereza, kuna Waislamu milioni 2.8 nchini humo kati ya watu milioni 64 nchini humo. Waislamu wameenea katika maeneo yote ya Uingereza na wamewakilishwa katika sekta zote za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

3639550

captcha