IQNA

Wanawake Washindi wa Nobel wamtaka Suu Kyi asitishe mauaji ya Waislamu Myanmar

18:46 - September 15, 2017
Habari ID: 3471174
TEHRAN (IQNA)-Wanawake waliowahi kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel wamemwandikia barua kiongozi wa chama tawala nchini Myanmar, Aung San Suu Kyi wakimtaka awatetee Waislamu wanaoendelea kuuawa nchini humo.

Jody Williams kutoka Marekani, MaireadMaguire wa Ireland Kaskazini, Leymah Gbowee wa Liberia naTawakkul Karman wa Yemen ni miongoni mwa washindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel waliomwandikia barua San Suu Kyi wakimtaka atekeleze majukumu yake ya kibinafsi ya kimaadili kwa kuwatetea Waislamu wa Rohingya wanaoendelea kuuawa nchini Myanmar.

Washindi hao wa Tuzi ya Amani ya Nobel wamemtuhumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Myanmar, Aung San Suu Kyi na watawala wa nchi hiyo kwamba, wamefumbia macho matatizo ya Waislamu wa nchi hiyo ambao maelfu miongoni mwao wameuawa na Mabidha na maelfu ya wengine kukimbia makazi na nyumba zao.

Barua hiyo ya washindi wa Tuzo ya Nobel imeashiria mauaji makubwa yanayofanywa dhidi ya Waislamu wa Rohingya, kubakwa na kunajisiwa wanawake na kuchomwa moto vijiji vyao na wamemtaka San Suu Kyi kuwatetea Waislamu hao.

Vilevile wamemtaka achukuemsimamo imara kuhusu mgogoro huo na kuwatambua rasmi Waislamu wa Rohingya kama raia wa Myanmar wenye haki kamili.

Wakati huo huo jumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu zimetangaza kwamba. Mshauri Mkuu wa Serikali ya Myanmar, Aung San Suu Kyi anapaswa kunyang'anywa Tuzo ya Amani ya Nobel kutokana na kunyamazia kimya mauaji ya kutisha yanayoendelea kufanyika nchini humo dhidi ya Waislamu.

Mauaji yasiyo na huruma ya serikali ya Myanmar kuwalenga Waislamu wa Rohingya yameibua hasira na malalamiko makubwa katika nchi mbalimbali za dunia.Maelfu ya Waislamu wa jamii ya Rohingya wameuawa katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na askari wa serikali kwa kushirikiana na Mabudha magaidi. Wimbi jipya la mauaji ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa Myanmar lilianza tarehe 25 Agosti mwaka huu ambapo zaidi ya Waislamu 6,000 wameuawa kwa umati.

3641976
captcha