Kwa mujibu wa Tawi la Houston la Baraza la Uhusiano wa Kiislamu Marekani, CAIR, mwanamke Mwislamu mwenye umri wa miaka 25, ambaye ni mzunngu na kwa kawaida huvaa vazi la Hijabu aliropoti kuwa, siku ya Alhamisi asubuhi alikuwa akiendesha gari kutoka sehemu anayofanya kazi
kama muuguzi wakati gari lilipomgonga kwa makusudi. Wakati alipotoka kuangalia uharibifu wa gari lake, aliyemgonga alitoka ndani ya gari lake na kumkejeli na kumtusi huku akitoa matamshi yenye chuki dhidi ya Uislamu.
Anasema anaamini uhasama huo ulitokana na kuwa alikuwa amevaa Hijabu. Anaongeza kuwa alipojairbu kurejea katiika gari lake ili kuepuka shari ya mtu huyo, ndipo alipodungwa kisu mkononi na begani. Anasema mpitanjia ndiye aliyemzuia mwanaume huyo kuendelea na hujuma yake hiyo.
Mwanamke huyo Mwislamu alirejea katika hospitali anapofanya kazi na kupata matibabu ya dharura. Mwenye kutekeleza hujuma hiyo anasemekana kuwa mwanamume mzungu alieykuwa na umri wa kati ya miaka 20-25.
Mkurugenzi wa CAIR Tawi la Houston Mustafa Carrol ametoa wito kwa yeyote mwenye habari kuhusu mtu huyo ambaye ametajwa kuwa hatari awasiliane na maafisa wa usalama.
3465497