Mufti wa Jimbo la Pahang Sheikh Dr. Abdulrahman Osman amesema Chuo Kikuu cha Al-Qur'an kitatoa fursa mbali mbali za kitaaluma kwa wanachuo ambao watahitimu ambao wote pia watatakiwa kuwa wamehifadhi Qur'ani Tukufu.
Katika Ilani ya 14 ya Uchaguzi Mkuu ya Chama cha Barisan Nasional, moja ya malengo makuu ni kuweza kuwa na Wamalaysia 125,000 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu sambamba na kuwa wamehitimu katika taaluma kama vile tiba, hisabati, na uhandisi ifikapo mwaka 2050.
Ilani hiyo inasema Qur'ani Tukufu inatoa muongozo kamili wa sekta zote za maisha na si tu katika masuala yanayohusiana na dini moja kwa moja bali hata katika taaluma kama vile sayansi, teknolojia n.k.
Mufti Osman anasema Qur'ani Tukufu inapaswa kutumika kikamilifu kwa maslahi ya Waislamu duniani.
3465511