Mapema mezi Machi Saudia ilitangaza kusitisha kwa muda Ibadah na Umrah baada ya kufunga misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina ikiwa ni katika jitihada za kuzuia kuenea ugonjwa wa corona.
Wiki Saudia imetangaza itaanza kupunguza zuio la usafiri baina ya miji miezi miwili baada ya sheria kali kuwekwa ili kukabiliana na janga la COVID-19. Aidha msikiti yote Saudia itafunugliwa kwa muda wa siku 20 na waumini wametakiwa kuzingatia kanuni za afya zilizowekwa ili kuzuia kuenea corona.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Saudia (SNA), kuanzia Juni 21 vizingiti vilivyowekwa vitaondolewa katika hatua tatu na kuishia kwa kuondolewa sheria ya kutotoka nje kote katika nchi hiyo isipokuwa katika mji mtakatifu wa Makka. Taarifa hiyo imesema Ibada ya Umrah, ambayo huwavutia mamilioni ya waumini kila mwaka kutoka maeneo yote ya dunia, itaendelea kusitishwa kwa muda usiojulikana. Waziri wa Hija wa Saudia pia amewataka Waislamu kwa sasa wasitishe mpango wa Ibada ya Hija hadi watakapokea maelekezo.
Idadi ya walioambukizwa COVID-19 nchini Saudia hadi kufikia sasa ni 74,795 na waliofariki ni 399.