IQNA

Wapalestina walaani vikali safari ya rais wa utawala wa Israel nchini Uturuki

10:02 - March 10, 2022
Habari ID: 3475026
TEHRAN (IQNA)- Harakati za mapambano ya Kiislamu ambazo zinapignaia ukombozi wa Palestina zimelaani vikali safari ya rais wa utawala haramu wa Israel Isaac Herzog nchini Uturuki wakati huu ambao Israel imeshadidisha hujuma dhidi ya Wapalestina.

Katika taarifa Jumatano, Harakati ya Jihadi Islami imelaani serikali ya Uturukikwa kumkaribisha Herzog nchini humo na kusema safari hiyo inajiri sambamba na kuongeza mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina katika Mji wa Quds (Jerusalem) na njama za Israel za kuuyahudisha mji huo. Jihad Islami imeongeza kuwa kitendo cha Uturuki kumkaribisha rais wa Israel ni usaliti kwa Quds na Palestina. Safari hii inaashiria kumpendelea adui na ni dhidi ya jihadi ya watu wa Palestina, imesema harakati ya Jihad Islami.

Nayo Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas imebainisha masikitiko yake kutokana na safari ya rais wa Israel nchini Uturuki. Katika taarifa Hamas imetoa wito kwa nchi za Kiarabu na Waislamu kutoupa utawala wa Kizayuni wa Israel fursa ya kujipenyeza katika eneo.  Aidha Hamas imesema inapinga vikali mawasiliano yoyote na adui anaykiuka matukifu ya Kiislamu na anayetekeleza njama za kuuyahudisha mji wa Quds na Msikiti wa Al Aqsa sambamba na kuwawekea mzingiro Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza.

Aidha  Hamas imesema utawala haramu wa Israel unaendele akuwashikilia mateka maelefu ya Wapaletina mbali na pia unawaua watoto na kuharibi nyumba za Wapalestina. Herzog aliwasili Uturuki Jumatano kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliokuwa unazorota baina ya Israel na Uturuki ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo na Rais  Recep Tayyip Erdogan.

Jana wananchi wa Uturuki walifanya maandamano makubwa ya kupinga na kulaani safari ya Herzog nchini humo.Katika maandamano hayo ya jana Jumatano, wananchi wa Uturuki waliokuwa wamekusanyika katika Medani ya Taksim walichoma moto bendera za utawala haramu wa Israel, na kulaani safari hiyo ya siku mbili ya rais wa utawala dhalimu wa Israel. Waandamanaji Uturuki walikuwa wamebeba mabango lililoandikwa "Hatutaki wauaji katika nchi yetu" huku wakiwa wambeba bendera za Palestina katika maandamano ya kupinga safari rais wa utawala haramu wa Israel nchini humo.

3478106

captcha