IQNA

Waislamu China

Rais Xi Jinping: Uislamu nchini China uendane na mwelekeo wa Kichina

12:18 - July 17, 2022
Habari ID: 3475512
TEHRAN (IQNA)- Rais Xi Jinping wa China amewataka viongozi kuongeza juhudi kuhakikisha kwamba Uislamu nchini China unaendana na kaununi za dini nchini humo na sera za kisoshalisti zinazofuatiliwa na Chama tawala cha Kikomunisti cha China.

Xi ameyasema hayo alipotembelea eneo lenye Waislamu wengi la Xinjiang, ambako vikosi vya usalama vya China kwa miaka kadhaa iliyopita vimefanya jitihada za kudhibiti maandamano ya Waislamu wa jamii ya Uygur.

Katika ziara yake ya siku nne katika eneo hilo iliyoanza Julai 12, Xi alikutana na maafisa wa serikali na amesisitiza kukuza hisia dhabiti za ujamaa katika taifa la China, kukuza mabadilishano, maingiliano na ushirikiano kati ya makabila mbalimbali.

Xi alisisitiza haja ya kuboresha uwezo wa utawala wa masuala ya kidini na kufikia ustawi bora wa dini zote nchini humo.

Kunapaswa kuwa na jitihada za kuhakikisha kuwa Uislamu nchini China unaendana na mwelekeo wa kitaifa wa China ambao ni wa Kisocialisti, alinukuliwa akisema na shirika la habari la serikali la Xinhua.

Mahitaji ya kawaida ya kidini ya waumini yanapaswa kuzingatiwa  na wanapaswa kuunganishwa kwa karibu karibu na chama na serikali, Xi aliongeza.

Katika miaka michache iliyopita, rais amekuwa akitetea sera ya kuhakikisha kuwa Uislamu nchini humo unaenda sambamba na  sera za Chama tawala cha Kikomunisti.

China imekuwa ikipambana na tuhuma kuwa imewaweka Waislamu wa Uygur kwenye kambi, ambazo Beijing inazitaja kama vituo vya kuondoa itikadi kali na elimu.

China inaishutumu Vuguvugu la Kiislamu la Turkistan Mashariki (ETIM) linalotaka kujitenga ambalo linaendehsa shughuli zake katika eneo hilo kwamba ndilo linalotekeleza mashambulizi mengi ya kigaidi.

Beijing pia inapuuzilia mbali madai ya mataifa ya Magharibi ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ZA Waislamu wa Uygur.

Hivi majuzi, Mkuu wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet alitembelea Xinjiang baada ya mchakato mrefu wa mazungumzo na Beijing kuchunguza madai ya kuwawekwa kambini Waislamu zaidi ya milioni ya Uygur wa umri tofauti kama sehemu ya ukandamizaji wa China dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu.

Mwishoni mwa ziara yake mjini Xinjiang tarehe 28 Mei, Bachelet alisema aliibua maswali na wasiwasi juu ya utumiaji wa hatua za kukabiliana na ugaidi na kuondoa itikadi kali na namna sheria hizo zinavyopelekea kukandamizwa  haki za jamii ya Uygur na Waislamu wengine walio wachache.

4071366

captcha