IQNA

Tauhidi Katika Qur'ani Tukufu /2

Matendo ya mwanadamu yatakavyobainika siku ya Kiyama

16:12 - November 16, 2022
Habari ID: 3476100
TEHRAN (IQNA) – Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ukweli wa matendo ya mwanadamu utadhihirika Siku ya Kiyama na kila mtu atalipwa au kuadhibiwa kwa matendo yake wenyewe.

Hujjatul Islam Mohammad Ali Khosravi, mtafiti wa masuala ya dini ametoa ufahamu kuhusu matokeo ya matendo mema na mabaya huko Akhera. Ufuatao ni mukhtasari wa kikao cha pili cha mjadala wake kuhusu Tauhidi.

Imam Ali (AS) anaitanguliza Qur'ani Tukufu kama "chemchemi ya nyoyo" kwani kitabu hiki kinapelekea kukua kwa moyo na kumuongoza mwanadamu kwenye matendo mema.

Kwa mujibu wa Qur'ani, Akhirah au siku ya Kiyama ni jibu kwa yaliyojiri katika dunia ya sasa. Tutafufuliwa Siku ya Kiyama jinsi tulivyoishi hapa duniani na tutashuhudia matokeo ya matendo yetu. Qur’ani Tukufu inasema: “Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliye ipotea zaidi Njia. (Surah Al-Isra', aya ya 72) Upofu hapa unamaanisha upofu wa moyo.

Kuna aya nyingine inayoelekeza kwenye dhana hiyohiyo: “ Enyi mlio kufuru! Msilete udhuru leo. Hakika mnalipwa mliyo kuwa mkiyatenda.” (Surah At-Tahrim, aya ya 7) Ina maana kwamba yale ambayo mtu atakutana nayo Siku ya Kiyama ni matendo yake wenyewe.

Aya haisemi kwamba watu wataongozwa kuelekea Peponi au Motoni, bali inasema ni matendo hayo ambayo yamedhihirika siku ya Kiyama na wanaadhibiwa au watalipwa kwa mujibu wa waliyoyatenda.

Kwa hiyo, Akhirah ndio ukweli wa dunia hii. Tunapaswa kuwa macho ili tuweze kuiona Akhirah katika ulimwengu huu na kwa njia hiyo tutaweza kutekeleza vitendao ambavyo vitamridhisha Mwenyezi Mungu.

captcha