Idara hiyo inayosimamiwa na Jordan ilisema uwepo mkubwa wa Waislamu kwenye eneo hilo takatifu wakati wa Ramadhani ulikuwa wa kushangaza mwaka huu licha ya ukubwa wa vizuizi vya utawala haramu wa Israel kwa lengo la kuwazuia waumini Wapalestina kutoka Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza
Wakati wa Mwezi Mtakatifu, waumini wenye umri wa miaka 12-55 kutoka Ukingo wa Magharibi walizuiwa kuingia katika mji mkongwe wa Quds, ambapo msikiti huo upo, huku idadi ndogo ya mamia kutoka kwa Ukanda wa Gaza wakiruhusiwa kuingia katika eneo la Msikiti wa Al Aqsa.
Sanjari na likizo ya Wayahudi ya Pasaka mapema Aprili, vikosi vya utawala vamizi wa Israel viliuvamia Msikiti wa Al Aqsa mara mbili na kuwafukuza maelfu ya waumini wa Kiislamu wakiwa katika ibada za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani sambamba na kuruhusiwa walowezi wa Kiyahudi wa Israel kuingia eneo hilo takatifu la Kiislamu na hivyo kulivunjia heshima. Uchokozi huo wa Israel ulilaniwa vikali kimataifa.
Tangu 2003, watawala wa Israel wamekuwa wakiruhusu walowezi ndani ya eneo la Msikiti wa Al Aqsa kila siku isipokuwa Ijumaa.
Idara ya Wakfu wa Kiislamu imeelezea kuwa uwepo wa walowezi katika msikiti wa al-Aqsa kuwa ni uchochezi.
Utawala wa Kizayuni wa Israel uliuteka mji wa Quds Mashariki, ambapo Msikiti wa Al-Aqsa upo, wakati wa vita vya siku sita mnamo 1967 katika harakati ambazo hazijawahi kutambuliwa na jamii ya kimataifa.
3483296