IQNA

Umoja wa Waislamu

Mkutano wa kukurubisha madhehebu za Kiislamu wafanyika Makka

6:22 - March 18, 2024
Habari ID: 3478533
IQNA - Jumuiya ya Waislamu Duniani (WML) imeandaa mkutano unaolenga kukuza maelewano kati ya madhehebu za Kiislamu.

Kongamano la Kimataifa la Kujenga Madaraja kati ya Madhehebu ya Kiislamu, limezinduliwa katika mji mtakatifu wa Makka siku ya Jumapili.

Wasomi, mamufti, wanafikra na shakhsia kutoka nchi tofauti za Kiislamu wamealikwa kushiriki katika hafla hiyo ya siku mbili, kwa mujibu wa tovuti ya MWL.

Miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano huo ni Abbas Khameyar,  mkuu wa masuala kitamaduni na kijamii katika Chuo Kikuu cha Dini na Madhehebu cha Iran, na mjumbe wa Baraza la Wanazuoni  Wataalamu la Iran Ayatullah Ahmad Mobaleghi.

Mkutano wa kwanza wa aina yake, utakuwa na midahalo yenye kusudi ili kuimarisha uhusiano kati ya shule za fikra za Kiislamu na kutimiza malengo yao ya pamoja.

Washiriki watajaribu kukuza udugu wa Kiislamu, ushirikiano na maelewano katika mitazamo juu ya masuala muhimu na malengo ya Umma wa Kiislamu.

Pia wanajadili hotuba zinazokabiliana, kauli mbiu na mbinu za kutengwa kwa misingi ya madhehebu, tovuti hiyo ilisema.

Mwishoni mwa mkutano huo, watatoa "Hati ya Kujenga Madaraja kati ya Madhehebu ya Kiislamu".

Mgogoro katika Ukanda wa Gaza, ambao umekuwa ukikabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari kwa zaidi ya miezi mitano, utakuwa pia kwenye ajenda ya mkutano huo, huku washiriki wakitarajiwa kutoa sauti ya mshikamano na Gaza na kusisitiza uungaji mkono wa kuundwa kwa taifa huru la Palestina mji mtakatifu wa Quds kama mji mkuu wake.

4205879

captcha