IQNA

Ramadhani katika Qur'ani /4

Kufunga au saumu katika mataifa ya kabla ya kuja kwa Uislamu

15:02 - March 19, 2024
Habari ID: 3478541
IQNA – Kwa mujibu wa Aya ya 183 ya Surah Al-Baqarah, kufunga pia ilikuwa ni wajibu kwa mataifa yaliyokuwepo kabla ya kuja kwa Uislamu.

Kulingana na yale yaliyomo katika Torati na Biblia za hivi sasa, Wayahudi, Wakristo na watu na mataifa mengine waliamua kufunga walipokabiliwa na huzuni au majonzi.

Tunasoma katika “Kamusi ya Biblia ya Kiajemi” ya James W. Hawkes kwamba kufunga kulikuwa jambo la kawaida katika kila taifa na dini nyakati za huzuni, misiba, na matukio yasiyotazamiwa.

Taurati inasema kuwa Nabii Musa (AS) alipokwenda mlimani, alikaa hapo siku arobaini mchana na usiku bila kula mkate wala kunywa maji.

Wayahudi walifunga walipotaka kutubu au kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Walifunga ili kuungama dhambi zao na kudhihirisha unyenyekevu wao na kutokuwa na msaada na kupata radhi za Mwenyezi Mungu.

Kulikuwa pia na mfungo maalum wa siku moja kati ya Myahudi na vile vile aina zingine za kufunga, Hawkes, aliandika.

Kulingana na Biblia, Nabii Isa a Yesu (AS) pia alifunga kwa siku arobaini: “Wakati huo Yesu aliongozwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na Ibilisi. Akafunga siku arobaini mchana na usiku kisha akaona njaa.” ( Mathayo 4:1-11 )

Na Kitabu cha Luka kinasema kwamba Wanafunzi pia walifunga.

Hawkes alisema katika “Kamusi ya Biblia ya Kiajemi” kwamba maisha ya waaminifu zamani yalikuwa yamejaa kujinyima furaha, kupitia magumu na kufunga.

Na Quran Tukufu inasema katika Aya ya 183 ya Surah Al-Baqarah:

“Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu".

3487579

captcha