IQNA

Jinai za Israel

Miili 190 yapatikana katika kaburi la umati hospitalini Gaza baada askari wa Israel kutoroka

20:48 - April 22, 2024
Habari ID: 3478717
IQNA - Takriban miili 190 imetolewa kwenye kaburi la umati katika Hospitali ya Nasser katika mji wa Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Miili hiyo ilipatikana kufuatia kuondoka kwa wanajeshi wa Israeli kutoroka mji huo mnamo Aprili 7 baada ya shambulio la kijeshi huko.

Taarifa zinasema wanawake na watoto ndio wengi katika kaburi hilo la umati.

Kulingana na taarifa,, karibu watu 500 wameripotiwa kutoweka kufuatia mashambulizi ya Israel dhidi ya Khan Younis.

Israel ilianzisha mashambulizi ya kikatili kwenye Ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 7, 2023.

Takriban Wapalestina 34,100 wameuawa shahidi, wengine wakiwa ni wanawake na watoto na wengine 77,000 wamejeruhiwa.

Vita vya Israel vimesukuma 85% ya wakazi wa Gaza kuhama makazi yao huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, wakati 60% ya miundombinu ya eneo hilo imeharibiwa au kuharibiwa, kulingana na UN.

3488030

Habari zinazohusiana
Kishikizo: jinai za israel
captcha