Chuo cha Masuala ya Kidini na Utafiti wa Kiislamu kinachofungamana na Chuo Kikuu cha Sharja katika Umoja wa Falame za Kiarabu kimeandaa kikao cha 'Nafasi ya Wakfu katika Harakati ya Kielimu ya Kiislamu' ambacho kimepangwa kufanyika tarehe 19 baadaye mwezi huu.
2011 May 05 , 13:02
Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran jioni ya leo amezindua rasmi Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran akisema kuwa fikra na kutafakari ndiko kunakomtofautisha mwanadamu na viumbe wengine.
2011 May 03 , 23:03
Nakala ya intaneti ya insaiklopidia ya Mwanamke na Utamaduni wa Kiislamu imezinduliwa katika Kitivo cha Anthropolojia (elimu ya binadamu) cha Chuo Kikuu cha California.
2011 May 02 , 21:47
Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya vitabu vya Kiislamu yamefunguliwa nchini Kuwait. Maonyesho hayo yanadhaminiwa na Jumuiya ya Marekebisho ya Kijamii ya Kuwait.
2011 Apr 30 , 17:02
"Siku ya Milango ya Wazi ya Uislamu" imepangwa kufanyika tarehe 30 Aprili katika mji wa Lyon nchini Ufaransa.
2011 Apr 27 , 18:18
Kikao cha kimataifa cha kuchunguza "Sira ya Mtume katika Maandishi ya Wataalamu wa Masuala ya Mashariki wa Kiholanzi kimeanza katika mji wa Fas nchini Morocco.
2011 Apr 26 , 17:43
Kikao cha 'Waislamu na Maisha ya Amani' kilifanyika hapo jana Jumapili katika mji wa kaskazini mwa Italia wa Brescia kwa udhamini wa Baraza la Ulaya la Maulama wa Morocco CEOM.
2011 Apr 18 , 11:42
Warsha ya utafiti wa Kiislamu imepangwa kufanyika tarehe 26 mei huko katika Chuo Kikuu cha Leeds nchini Uingereza.
2011 Apr 13 , 17:44
Maonyesho ya kwanza ya ufumaji na bidhaa za kibiashara za Kiislamu yamepangwa kufanyika tarehe 5 Mei katika jumba la maonyesho la Francisca Galloway mjini London.
2011 Apr 10 , 12:12
Filamu ya kweli kuhusu mwanakaligrafia bora zaidi wa ulimwengu wa Kiislamu duniani itatengenezwa hivi karibuni na Shirika la Chapa na Usambazaji wa Qur'ani Tukufu la Mfalme Fahd mjini Madina.
2011 Apr 07 , 12:06
Mpango wa 'Ujue Uislamu' umeanza kutekelezwa leo Jumanne katika Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kiislamu ya chuo hicho.
2011 Apr 05 , 17:47
Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu yameanza leo Jumatatu huko katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad.
2011 Apr 04 , 16:50
Maonyesho ya Historia ya Makka ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda wa wiki moja katika hoteli ya as-Shuhadaa huko katika mji mtakatifu wa Makka yalimalizika siku ya Jumapili.
2011 Mar 29 , 10:46