Filamu ya Maafa kutoka Gaza, Siku Inayofuata" (Gaza-Strophe, le jour d’après) iliyotengenezwa na Samir Abdullah na Khairuddin Mabruk imeshinda tuzo ya filamu bora zaidi matukio ya kweli ya tamasha ya Tuzo ya Kimataifa ya Filamu za Matukio ya Kweli na Ripoti ya Meaditerania" iliyofanyika katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.
2010 Dec 11 , 17:07
Kongamano la Tatu la Teknolojia ya Mawasiliano chini ya anwani ya, 'Mada za Kiislamu na Kiarabu katika Intaneti" litafanyika Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia.
2010 Dec 09 , 12:57
Kitabu chenye anwani ya "Wadhifat al Majlisi Husseini (AS)" au 'Risala ya Majlisi ya Husseini" kimechapishwa katika mji mtakatifu wa Karbala.
2010 Dec 09 , 12:55
Tamasha la pili la kimataifa la filamu za matukio ya kweli (documentary) katika Ukanda wa Gaza lilianza jana kwa ujumbe wa kushikamana na wananchi wa Palestina. Tamasha hilo linazikutanisha pamoja nchi 14 za Kiarabu na kigeni.
2010 Dec 08 , 20:18
Kikao cha kimataifa cha kumuadhimisha Hadhrat Ali Asghar (as) kimepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 10 Disemba nchini Saudi Arabia. Kikao hicho kitafanyika katika Husseiniya ya Zeinabiyya katika mji wa Awamiya katika mkoa wa Qatif.
2010 Dec 08 , 19:00
Chuo cha kidini cha al-Ghadir kimefunguliwa katika mji wa Sitra nchini Bahrain kwa kuhudhuriwa na ujumbe wa Baraza la Maulama wa Kishia la Bahrain.
2010 Dec 07 , 16:56
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO na Jumuiya ya Kimataifa ya Familia zimetiliana saini hati ya ushirikiano katika kikao kilichofanyika Paris, Ufaransa.
2010 Dec 06 , 18:02
Kitabu chenye anwani ya "Mazungumzo baina ya Dini na Tamaduni" kilichoandikwa na Mohammad Habib Kébé mhadhiri wa fasihi kimechapishwa nchini Senegal.
2010 Dec 04 , 13:56
Maonyesho ya 'picha za Ashura' yaliyoanza siku ya Alkhamisi katika Kituo cha Utamaduni cha Cem Karaca katika eneo la Bakirkoy mjini Istanbul yamewavutia wananchi wengi wa Uturuki.
2010 Dec 04 , 13:49
Kongamano la kumuenzi Sheikhul Ishraq litafanyika mapema mwakani nchini Syria kwa hima ya Chuo Kikuu cha Tehran na Taasisi ya Utafiti wa Kifalsafa ya Iran.
2010 Dec 02 , 09:21
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (ISESCO) linatayarisha hati mbili za Kiislamu zinazobeba anwani ya: "Mbinu za Sayansi, Falsafa, Fasihi na Sanaa kati ya Ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi" na Ustaarabu wa Kiislamu katika Kioo cha Dunia, Upeo wa Falsafa".
2010 Nov 21 , 16:02
Idara ya Ustawi wa Kiutamaduni ya Baraza Kuu la Akiolojia la Misri imeandaa kongamano la 'Uchoraji katika Uislamu'.
2010 Nov 21 , 14:40
Maonyesho ya picha nadra za kale za al-Kaaba Tukufu na maeneo mengine matakatifu ya mji mtukufu wa Makka, picha ambazo zinarejea nyuma katika historia hadi karne ya 19 Milaadia, yanaendelea katika mji wa Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.
2010 Nov 20 , 11:00