Kitabu chenye anwani ya "Mtume Muhammad SAW katika Ukristo" kilichoandikwa na hayati Ahmad Deedat kimetarjumiwa kwa lugha ya Kihausa nchini Nigeria.
2010 Dec 30 , 12:41
Maonyesho ya “Turathi ya Qur’ani, Ujumbe wa Amani” yamepangwa kufanyika katika miezi ya mwanzoni mwa mwaka ujao katika Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu katika mji wa Oakland Jimboni California Kaskazini.
2010 Dec 29 , 14:34
Kikao cha sita katika mfululizo wa vikao kuhusu Sira ya Mtume SAW kimepangwa kufanyika katika Chuo cha Kidini cha Narjes katika mji mtakatifu wa Mash'had kaskazini mashariki mwa Iran.
2010 Dec 29 , 12:56
Mwenyekiti wa Baraza la Mkoa wa Najaf nchini Iraq ametoa wito wa kufanyika mkutano wa kimataifa wa kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu katika mji mtakatifu wa Najaf kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC.
2010 Dec 28 , 17:28
Kikao cha Kumi cha Baraza la Ushauri Kuhusu Utekelezaji Mkakati wa Utamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu kimefanyika Disemba 24-25 katika Rabat mji mkuu wa Morocco.
2010 Dec 26 , 12:57
Maonyesho ya muujiza wa kisayansi wa Qurani na Sunnah ya Mtume SAW yanafanyika mjini Doha Qatar.
2010 Dec 21 , 12:46
Maonyesho ya kazi za sanaa ya kale na ya kisasa ya Kiislamu yanafanyika hivi sasa katika jumba la makumbusho la Haus der Kunst katika mji wa Munich nchini Ujerumani.
2010 Dec 20 , 18:04
Toleo la 24 la jarida la Kiarabu la Al Bayan limejadili kwa kina mkakati wa kuyakurubisha madhehebu ya Kiislamu.
2010 Dec 14 , 16:10
Jumba la makumbusho ya Kiislamu la Baituil Qur’ani la Bahrain limechapisha athari za sanaa ya Kiislamu ya Iran katika kalenda ya mwaka mpya wa Miladia wa 20011.
2010 Dec 13 , 10:12
Jumuiya ya Ahlul Beit (as) ya Uingereza imezungumzia tukio la Ashura katika mtandao wake kama mojawapo ya njia za kubainisha na kueneza mafundisho yanayotokana na mapambano ya Imam Hussein (as) huko Karbala.
2010 Dec 12 , 16:46
Kongamano la Kwanza la Wakuu wa Maktaba za Vyuo Vikuu vya Nchi za Kiislamu kitafanyika Cairo kuanzia Disemba14-16 katika Chuo Kikuu cha Cairo nchini Misri.
2010 Dec 12 , 08:46
Duru ya 15 ya mafunzo maalumu ya kidini kwa maimamu na waadhini wa misikiti yameanza leo Jumamosi katika mji wa al-Uneiza nchini Saudi Arabia na yamepangwa kuendelea kwa muda wa siku nne.
2010 Dec 11 , 18:02
Filamu ya Maafa kutoka Gaza, Siku Inayofuata" (Gaza-Strophe, le jour d’après) iliyotengenezwa na Samir Abdullah na Khairuddin Mabruk imeshinda tuzo ya filamu bora zaidi matukio ya kweli ya tamasha ya Tuzo ya Kimataifa ya Filamu za Matukio ya Kweli na Ripoti ya Meaditerania" iliyofanyika katika mji wa Marseille nchini Ufaransa.
2010 Dec 11 , 17:07