Fadhila na shaksia ya Imam Ali (as) itabainishwa na kuarifishwa katika kikao maalumu kilichopangwa kufanyika hapo siku ya Jumatatu Juni Nne katika Kituo cha Rasul al-Akram mjini Antananarivo nchini Madagascar, kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Imam huyo mtukufu (as).
2012 May 30 , 16:46
Maonyesho ya kaligrafia ya Kiislamu yalifanyika jana Jumanne katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu cha Islamabad IIUI.
2012 May 30 , 16:45
Kwa mara ya kwanza polisi ya Russia imefundishwa misingi ya mafunzo ya Kiislamu. Kikao cha kwanza kwa masomo hayo kilifanyika siku ya Ijumaa katika mkoa wa Nizhny Novgorod ambapo polisi wapatao 60 walishiriki.
2012 May 28 , 12:01
Tarjuma ya Kiswahili ya As Sahifat ul Kamila as Sajjadiya imetarjumiwa kwa lugha ya Kiswahili na Taasisi ya Al Itrah ya Tanzania.
2012 May 14 , 12:33
Wanaakiolojia wamefanikiwa kuchimbua kasri ya kale zaidi ya Kiislamu Iran walipokuwa wakifukua mji wa kale wa Estakhr katika mkoa wa Fars.
2012 May 10 , 17:10
Maonyesho ya vitabu vya Kiislamu yamepangwa katika mji mkuu wa Nigeria Abuja kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa kusoma nchini humo.
2012 May 03 , 12:01
Kongamano la kila miaka miwili la Iran na Malaysia kuhusu Uislamu litafanyika mjini Tehran mwaka huu chini ya anwani ya, 'Uadilifu katika Uislamu'.
2012 May 02 , 19:28
Askari usalama wa Mauritania wamemtia nguvuni Biram Old Abidi, Kiongozi wa Jumuiya ya Mapambano kwa Ajili ya Ukombozi kwa tuhuma ya kuvunjia heshima vitabu vya Kiislamu.
2012 Apr 29 , 18:00
Maombolezo ya kuuawa shahidi Bibi Fatma az-Zahra (as) binti wa Bwana Mtume (saw) yalifanyika hivi karibuni mjini Ujerumani ambapo wafanyakazi wa ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Wairani na Waislamu wengine wapenzi wa Ahlul Beit (as) wanaoishi nchini humo walishiriki.
2012 Apr 29 , 17:37
Msanii wa India Anil Kumar Chauhan ametumia zaidi ya thuluthi moja ya umri wake kwa ajili ya kaligrafia ya aya za Qur'ani Tukufu na kuchora aya hizo misikitini.
2012 Apr 21 , 20:06
Serikali ya Uganda imesisitiza juu ya ulazima wa kuungwa mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.
2012 Apr 05 , 11:37
Msanifu majengo wa Iran ameibuka mshindi katika mashindano ya kimataifa ya 'Kuifanya Makka iwe Maridadi' yaliyoandaliwa na Saudi Arabia kwa lengo la kuuboresha mji mtakatifu zaidi katika Uislamu.
2012 Mar 12 , 13:49
Semina ya Kimataifa kuhusu 'Nafasi ya Wairani katika Ustaarabu wa Kiislamu' itafanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Indonesia.
2012 Mar 03 , 20:01