IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Jordan

17:38 - April 11, 2016
Habari ID: 3470239
Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Jordan kwa ajili ya wanawake yameanza Jumapili kwa kuhudhuriwa na Waziri wa Awqaf nchini humo pamoja na mabalozi wa nchi kadhaa.

Wawakilishi wa nchi mwenyeji, Misri, Bosnia na Herzegovina, Bahrain na Malaysia walikuwa wa kwanza kushiriki katika mashindano hayo.

Mshiriki wa Iran Sama Babayi, anatazamiwa kuingia katika jukwaa leo katika kitengo cha kuhifadhi Qur’ani kikamilifu. Bi. Babayi, ambaye ni kutoka Tehran, alishika nafasi ya kwanza katika kuhifadhi Qur’ani nzima katika mashindano ya kitaifa ya 38 ya Qur’ani ya Iran na kwa msingi huo akateuliwa kuwakilisha Iran katika mashindano hayo.

Mashindano hayo yameandaliwa na Wizara ya Awqaf na Masuala ya Kiislamu Jordan ambapo kuna washiriki wakiwemo wa vitengo vya kuhifadhi na kusoma kutoka nchi mbali mbali.

Mashindano baina ya wanawake yataendelea hadi Aprili 14 huku yale ya wanaume yakitazamiwa kuanza Juni 25.

Mahmoud Babakhan atawakilisha Iran katika mashindano ya wanaume.


3459499


Kishikizo: jordan mashindano
captcha