IQNA

Harakati za Qur'ani

Wizara ya Wakfu Jordan imechapisha Misahafu milioni moja

19:51 - January 22, 2024
Habari ID: 3478237
IQNA - Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Jordan imechapisha nakala milioni moja za Qur'ani Tukufu tangu ilipoanzishwa mwaka 1968.

Misahafu hiyo imesambazwa katika misikiti na shule za Jordan pamoja na baadhi ya nchi nyingine za Kiislamu, wizara hiyo imesema katika taarifa.
Aidha wizara hiyo imesema viongozi wa nchi hiyo wamefadhili uchapishaji wa baadhi ya Misahafu hiyo ambayo imepewa anuani za wafadhili. Misahafu hiyo ni pamoja na Mus’haf Al-Bayt, Mus’haf Hashimi, na Mus’haf Malik Hussein.
Wakati huo huo, Waziri wa Wakfu Mohammad Ahmad Muslim Al Khalayleh alisema awali kwamba toleo jipya la Mus’haf Hashimi linatayarishwa na hivi karibuni litachapishwa na wizara hiyo.
Vile vile amesisitiza kukua kwa shughuli za Qur'ani nchini Jordan na juhudi za kuhudumia Kitabu Kitukufu na kueneza mafundisho ya Qur'ani.
Mpango maalum wa wakfu umepangwa kuzinduliwa kwa ajili ya kusaidia uchapishaji wa nakala za Qur'ani Tukufu alibainisha zaidi.
Mbali na kufanya programu za Qur'ani nchini Jordan, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu inaunga mkono shughuli za Qur'ani katika Msikiti wa Al-Aqswa katika mji mtakatifu wa al-Quds (Jerusalem), Palestina, kwani Jordan ndio msimamizi rasmi wa maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo jijini Al Quds.

3486898

Habari zinazohusiana
captcha