IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran watangazwa

12:13 - January 19, 2023
Habari ID: 3476428
TEHRAN (IQNA) - Jopo la waamuzi wa Mashindano ya 45 ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran limetangaza majina ya washindi katika sehemu ya wanaume na wanawake ya mashindano hayo.

Mashindano hayo yalianza 12 Januari huko Ahvaz, mji mkuu wa jimbo la Khuzetsan kusini magharibi mwa nchi.

Washindani walishinda tuzo ya juu katika kategoria za usomaji wa Qur'ani, Tarteel, kuhifadhi Juzuu 20 za Qur'ani Tukufu na pia kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu.

Siku ya Jumatano, jopo la waamuzi lilitaja washindi katika kategoria tofauti.

Kulingana na jopo hilo, Hadi Esfidani kutoka Mkoa wa Khorasan Razavi alinyakua tuzo ya juu katika kitengo cha usomaji cha wanaume.

Omid Reza Rahimi kutoka Gilan alikuja wa kwanza katika kuhifadhi Qur'ani nzima, wakati Mohammad Mehdi Rezaei na Mohammad Poursina, wote kutoka Isfahan, walishinda taji la juu katika kuhifadhi Juzes (sehemu) 20 za Quran na usomaji wa Tarteel, mtawalia.

Kuhusu sehemu ya wanawake, Roya Fazaeli kutoka Khorasan Razavi, Fatemeh Mohammadi Dehnouki kutoka Fars, Ghazaleh Soheilizadeh kutoka Alborz na Adeleh Sheikhi kutoka Markazi walikuja wa kwanza katika kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi Juzuu 20, usomaji wa Qur'ani na Tarteel, mtawalia.

Mashindano hayo huandaliwa kila mwaka na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada Iran kwa kushirikisha wanaharakati wakuu wa Qur'ani kutoka kote nchini. Mashindano hayo hulenga kugundua vipaji vya Qur'ani na kuimarisha ufahamu na utekelezaji mafundisho ya Qur'ani Tukkufu katika jamii.

  4115494

captcha