Wizara hiyo ilisema washirikki 85 kutoka nchi za mabara tofauti wamechukua kozi hizo. Wanatoka Urusi, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Nigeria, Kongo, na Ivory Coast miongoni mwa wengine. Wanapokea masomo juu ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu, fikra za Qur'ani, tovuti ya Akhbar al-Yawm iliripoti.
Wale watakaofaulu vyema masomo hayo watapata vyeti vya kuhifadhi robo ya Quran Tukufu. Kutumia mtandao kwa ajili ya kufundisha Qur'ani na kutoa kozi za Qur'ani mtandaoni kumeendelezwa katika miaka ya hivi karibuni kwani huwapa watu kote ulimwenguni fursa ya kujifunza Qur'ani Tukufu Nchini Misri, wizara ya Awqaf ina jukumu la kuandaa, kuratibu na kusimamia shughuli za Qur'ani na kidini.
4146218