IQNA

Jordan ina zaidi ya Vituo 2000 vya Qur'ani vya majira ya joto

18:36 - September 06, 2021
Habari ID: 3474264
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Jordan wa Wakfu, Masuala ya Kiislamu na Maeneo Matakatifu amesema kuna zaidi ya vituo 2,000 vya Qur'ani vinavyotumika wakati wa msimu wa joto nchini humo.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimu ya wanafunzi wa vituo hivyo, Muhammad Al-Khalayilah, amesema kwamba wizara yake inajaribu kukuza kizazi kulingana na mafundisho ya Qur'ani na Uislamu.

Alisema kuwa kuna zaidi ya vituo 2000 vya majira ya joto vya Qur'ani katika sehemu tofauti za nchi zinazofanya kazi kikamilifu chini ya uangalizi wa maimamu wa misikiti, wahubiri wa kiume na wa kike na wataalam katika nyanja za Qur'ani na dini.

Ameongeza kuwa,  wizara inazingatia walemavu na inajaribu kubuni programu maalum za Qur'ani kwa kikundi hiki pia..

Pia, mkurugenzi wa Ofisi ya Wakfu ya Amman alisema kuwa wizara hiyo inakusudia kusaidia kumbukumbu za Quran kwa kuandaa kozi za Qur'ani za majira ya joto na mashindano ya kidini.

3994479

Kishikizo: jordan qurani tukufu
captcha