IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Majaji 32 katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

19:08 - February 13, 2023
Habari ID: 3476554
TEHRAN (IQNA) - Wataalamu wa Qur'ani kutoka Iran na nchi nyingine nane watahudumu katika jopo la waamuzi katika awamu ya mwisho ya Awamu ya 39 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.

Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada kimewataja wajumbe wa majopo hayo katika sehemu za wanaume na wanawake.

Kwa mujibu wa kituo hicho, kutakuwa na wataalamu 22 wa Qur'ani wa Iran na 10 kutoka nchi nyingine ambazo ni Lebanon, Kuwait, Bahrain, Iraq, Afghanistan, Jordan, Syria na Tajikistan.

Abbas Salimi atakuwa mwenyekiti wa jopo katika sehemu ya wanaume huku Maedeh Adibzadeh akiongoza jopo la sehemu ya wanawake.

Duru ya mwisho itaanza katika sherehe za ufunguzi Jumamosi, Februari 18, sambamba na Siku ya Maba’ath (kuashiria kuteuliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) kama mjumbe wa mwisho wa Mwenyezi Mungu).

Makari 52 na wahifadhi kutoka nchi 32 watachuana katika hatua ya fainali, kwa mujibu wa waandaaji.

Kategoria za shindano hilo ni pamoja na kusoma, kuhifadhi na tarteel kwa wanaume na kuhifadhi na tarteel kwa wanawake.

Jumla ya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani Tukufu 149 kutoka nchi 80 wakiwemo wanaume 114 na wanawake 35 walishiriki katika duru ya kwanza.

Kauli mbiu ya duru ya mwaka huu ya mashindano, kama yam waka jana, ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", ushuhuda wa umuhimu ambao Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa suala la umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali.

4121518

captcha