IQNA

Wapalestina watatu wauawa shahidi katika oparesheni dhidi ya Wazayuni Quds Tukufu

11:26 - July 14, 2017
Habari ID: 3471066
TEHRAN (IQNA)-Wapalestina watatu wamepigwa risasi na kuuawa katika oparesheni dhidi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji unaokaliwa kwa mabavu wa Quds.

Taarifa zinasema kumejiri ufyatulianaji risasi baina ya wanajeshi Wazayuni na Wapalestina karibu na mlango wa Bab al-Asbat katika Msikiti wa al Aqsa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambapo Wapalestina watatu wameuawa shahidi.

Wanajeshi wawili wa utawala wa Kizayuni wa Israel pia wameangamizwa katika oparesheni hiyo.

Aidha baada ya kujiri mapigano hayo katika eneo la Msikiti wa Al Aqsa, utawala wa Kizayuni umefunga milango yote ya msikiti huo na Wapalestina hawana ruhusa kuingia hapo.

Duru za Palestina zinadokeza kuwa, katika tukio hilo, wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel wamemkamata mwanamko moja na watoto watatu Wapalestina katika Bab al-Asbat.

Aidha wanajeshi wa Kizayuni sasa wameutangaza msikitiwa al Aqsa kuwa eneo la kijeshi na wamewazuia Wapalestina kuswali sala ya kila siku ya Ijumaa hapo.

Oparesheni hiyo ya Palestina ni sehemu ya Intifadah au mwamako wa tatu wa Wapalestina uliopewa jina la Intifadha ya Quds na ulianza Oktoba mwaka 2015 katika Msikiti wa al Aqsa. Intifadha hiyo ilianza kufuatia hujuma dhidi ya msikiti huo ambazo zimekuwa zikitekelezwa mara kwa mara na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni pamoja na walowezi wa Kizayuni. Katika Intifadha hii hadi sasa Wapalestina zaidi ya 330 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni.

3618649


captcha