IQNA

Nchi za Kiislamu zalaani hatua ya Israel kuufunga Msikiti wa al-Aqsa

18:57 - July 15, 2017
Habari ID: 3471067
TEHRAN (IQNA)-Ulimwengu wa Kiislamu umelaani hatua ya utawala haramu wa Israel ya kuufunga Msikiti wa al Aqsa katika mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu baada ya oparesheni ya Wapalestina dhidi wanajeshi wa Kizayuni karibu na msikiti huo.

Katika oparesheni hiyo ya Ijumaa Wapalestina waliwapiga risasi na kuwaangamiza wanajeshi wawili wa utawala wa Kizayuni wa Israel na baada ya hapo askari wa Kizayuni waliokuwa hapo waliwapiga risasi na kuwaua shahidi vijana watatu Wapalestina.

Kufuatia tukio, hilo utawala wa Kizayuni wa Israel uliufunga mskiti wa Al Aqsa na kuwazuia Waislamu kusali sala ya Ijumaa na hadi sasa msikiti huo umefungwa. Aidha Wazayuni walimkamata kwa muda Imamu wa Msikiti wa Al Aqsa Sheikh Muhammad Hussein aliyesalisha Ijumaa barabarani nje ya msikiti huo. Hii ni mara ya kwanza kwa sala ya Ijumaa kutosaliwa katika Msikiti wa Al Aqsa tokea mwaka 1969.

Jumuiya ya Nchi za Kiarbau imelaani vikali hatua hiyo ya Israel na kuitaja kuwa hatari kwani inaweza kuchochea ugaidi na misimamo mikali. Jordan ambayo ni msimamizi wa kimatiafa wa uwanja wa Msikiti wa Al Aqsa imetaka msikiti huo ufunguliwe haraka na imeutaka utawala wa Kizayuni uache kuchukua hatua zenye lengo la kubadilisha muundo wa Quds Tukufu au Msikiti wa Al Aqsa.

Kwa upande wake Hussein Amir Abdulahian, Katibu Mkuu wa Kongamano la Kimataifa la Palestina ambaye pia ni Mshauri wa Spika wa Bunge la Iran amelaani vikali hatua ya Israel ya kuufunga msikiti wa Al Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu. Abdullahian amesema watu wanaodhulumiwa Palestina wanapaswa kutumia kila mbinu kutetea haki zao kimataifa. Aidha amesema utawala wa Kizayuni wa Israel unalenga kuubadilisha mji mkuu wake kutoka Tel Aviv hadi Quds Tukufu na kuongeza kuwa uungaji mkono wa Marekani na kimya cha baadhi ya tawala za Kiarabu ni mambo ambayo yameufanya utawala wa Kizayuni upate kiburi zaidi. Aidha amesea njia pekee ya taifa la Palestina kupata haki zake ni kupitia mapambano na muqawama dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Oparesheni hiyo ya Ijumaa ya Wapalestina dhidi ya askari wa Kizayuni ni sehemu ya Intifadah au mwamako wa tatu wa Wapalestina uliopewa jina la Intifadha ambapo Intifahda ya sasa ni ya tatu na imepewa jina la Intifadha ya Quds NA na Ilianza Oktoba mwaka 2015 katika Msikiti wa al Aqsa. Intifadha hiyo ilianza kufuatia hujuma dhidi ya msikiti huo ambazo zimekuwa zikitekelezwa mara kwa mara na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni pamoja na walowezi wa Kizayuni. Katika Intifadha hii hadi sasa Wapalestina zaidi ya 330 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel huku wengine zaidi ya 24000 wakijeruhiwa.

3463351

captcha