IQNA

Fatwa ya Alim wa Iraq kuhusu Saumu ya Ramadhani wakati wa janga la corona

19:54 - April 15, 2020
Habari ID: 3472669
TEHRAN (IQNA) – Mwanazuoni wa ngazi za juu wa Kiislamu katika madhehebu ya Shia nchini Iraq ametoa Fatwa kuhusu kufunga saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati huu wa janga la ugonjwa wa corona au COVID-19.

Ayatullah Bashir Hussein Najafi ametoa Fatwa baada ya swali (istifta) kuhusu hofu kuwa saumu inaweza kuongeza uwezekano wa mtu kuambukizwa COVID-19. Alim huyo amenukuliwa na Televisheni ya Al-Sumaria akisema iwapo Mwislamu ana yakini kuwa saumu itapelekea aambukizwe corona, basi si wajibu kwake kufunga.

Hatahivyo mwanazuoni hiyo ameongeza kuwa, hakuna ushahidi wowote kamilifu wa kitiba unaoonyesha kuwepo uhusiano baina ya saumu na maambukizi ya COVID-19. Aidha Ayatullah Bashir Hussein Najafi ameashiria hadithi ya Mtume Muhammad SAW aliposema: “Funga Upate Afya” na kusema kufunga sumu ya Mwezi Mtukufu  kunapaswa kuzingatiwa kuwa ni kursa ya kuzuia magonjwa ukiwemo ugonjwa wa COVID-19.

Fatwa ya Alim wa Iraq kuhusu Saumu ya Ramadhani wakati wa janga la corona

3891833

captcha