IQNA

Uislamu na Elimu

ISESCO kuanzisha hazina ya kwasaidia wasomi wa Ulimwengu wa Kiislamu

13:23 - December 22, 2022
Habari ID: 3476288
TEHRAN (IQNA)- TEHRAN (IQNA) – Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni Duniani (ISESCO) linapanga kuanzisha mfuko kwa ajili ya kusaidia wasomi na watu mahiri katika ulimwengu wa Kiislamu.

Hii ilitangazwa katika mkutano wa hivi karibuni wa mawaziri wa nchi wanachama wa shirika hilo ambao ulifanyika Rabat, mji mkuu wa Morocco, ili kujadili utaratibu wa kusaidia watu wenye vipaji wa ulimwengu wa Kiislamu.

Katibu Mkuu wa ISESCO Salim Mohammed Al-Malik alisema mfuko huo utasaidia kukuza ubunifu miongoni mwa watu katika nchi wanachama.

Alisema wanachama wa shirika hilo wameunga mkono kwa kiasi kikubwa mpango huo.

ISESCO hapo awali ilianzisha mipango mingi ya kusaidia masomo ya utafiti katika ulimwengu wa Kiislamu haswa miongoni mwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

Shirika hilo pia limezindua tuzo katika uwanja wa masomo ya kielimu juu ya miujiza ya Qur'ani Tukufu.

ISESCO ni shirika la kimataifa linalofanya kazi ndani ya mfumo wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na lilianzishwa Mei mwaka 1979. ISESCO ndio taasisi kubwa zaidi ya Kiislamu katika uga wa kimataifa inayoshughulikia masuala ya elimu, sayansi na utamaduni.

4108708

 

captcha