Kwa msingi huo, maonyesho hayo yataendelea kwa muda wa mwaka moja katika makao makuu ya ISESCO. Maonyesho hayo yalizinduliwa Novemba 17, 2022, tovuti ya ISESCO iliripoti.
Hii ni mara ya kwanza kwa maonyeso hayo kufanyika nje ya Saudi Arabia kwani yameuwa yakifanyika katika mji wa Madina Al Munawarah.
Tangu ufunguzi wake wa umma mnamo Novemba 28, 2022, maonyesho hayo yamevutia wageni karibu milioni moja na nusu, kutoka wakiemo raia wa Moroko na wageni wa kimataifa.
Wasomi na wanafikra maarufu kutoka ulimwengu wa Kiisilamu wametembelea maonyesho hayo ambayo ni marejeo muhimu kwa wale wanaotaka kuongeza uelewa wao juu ya wasifu na mafundisho ya Nabii Muhammad (PBUH).
Maonyesho yanalenga kufikisha ujumbe wa Uislamu na maadili yake ya haki, amani, rehema, uvumilivu, umoja na misimamo ya wastani, yote ambayo yameingizwa sana katika Qur’ani Tukufu, Sunnah ya Mtume SAW na historia ya Uislamu.