IQNA

Chuki dhidi ya Uislamu

Msikiti wa Oxford walengwa katika 'Hujuma ya Chuki dhidi ya Uislamu' baada ya kuunga mkono Palestina

16:51 - October 30, 2023
Habari ID: 3477812
LONDON (IQNA) - Msikiti mmoja huko Oxford umelengwa na "shambulio la chuki dhidi ya Uislamu na kigaidi" kufuatia jamii ya Waislamu kuunga mkono Wapalestina wanaoteswa na Israel huko Gaza.

Pipa la petroli lenye maneno "IDF RULE" na "IDF", ya kuashiria Jeshi la Israel, lilitupwa juu ya ukuta wa Msikiti wa Kati wa Oxford mnamo Oktoba 28.

Polisi wametaja tukio hilo kuwa ni uhalifu wa chuki na wanashirikiana na msikiti na jamii ya eneo hilo kuhakikisha usalama wao.

Baraza la Misikiti lilitoa tamko, likilaani tukio hilo kama "shambulio la chuki dhidi ya Uislamu na la kigaidi" la "gaidi mmoja".

Taarifa hiyo ilisema kuwa msikiti huo umeweka bendera za Palestina kuzunguka majengo yake ili kuonyesha "uungaji mkono wake usioyumba" kwa watu wa Palestina, ambao wanakabiliwa na mauaji "ya kiholela na haramu" yanayofanywa na Israel.

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa msikiti huo hautatishwa na shambulio hili na utaendelea kutekeleza haki yake ya kidemokrasia na mshikamano wake na Wapalestina.

Polisi wa Bonde la Thames walisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika hujuma, lakini wamesema inaweza kuwa inahusiana na mzozo unaoendelea wa Israel na Gaza".

Naibu Inspekta James Holden-White alisema kuwa wanafanya doria zaidi katika eneo hilo na kuuhakikishia msikiti na jamii usalama wao. Aidha alisema kwa yeyote mwenye taarifa za tukio hilo awasiliane na polisi.

Shambulio hilo linakuja huku kukiwa na ongezeko la jinai za chuki dhidi ya Uislamu katika baadhi ya nchi za Magharibi, zikiwemo Uingereza na Marekani huku kukiwa na vita vilivyoanza Oktoba 7.

Inafaa kuashiria hapa kuwa katika kukabiliana na jinai za Wazayuni, vikosi vya muqawama vya Palestina vilianza operesheni ya "Tufani ya Al Aqsa" ukanda wa Ghaza dhidi ya ngome za utawala wa Kizayuni  wa Israel kuanzia Jumamosi, Oktoba 7, 2023.

Tangu kuanza kwa operesheni hiyo, jeshi la Kizayuni, ambalo halina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji wa muqawama, limekuwa likishambulia kwa mabomu maeneo ya raia, hospitali, vituo vya kidini na shule huko Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Afya ya Palestina, zaidi ya Wapalestina 8000 wameuawa shahidi na wengine takriban 20,000 wamejeruhiwa tangua kunza jinai mpya ya mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika ukanda wa Ghaza. Aghalabu ya waliopoteza maishani wanawake na watoto.

3485793

Habari zinazohusiana
captcha