IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Dua za Kila Siku za Mwezi wa Ramadhani- Siku ya 19

Dua hizi za kila siku za Mwezi wa Ramadhani husomwa toka mwanzo ya tarehe mosi Ramadhani hadi siku ya mwisho katika mwezi huu mtukufu. Kila dua ina siku yake, na inaweza kusomwa mara nyingi kadiri ya uwezo wa mtu mwenyewe.

Ee Mwenyezi Mungu! Niongezee fungu langu la baraka za mwezi huu, na Unisahilishie njia ya kuyafikia mema ya mwezi huu, wala Usininyime kukubaliwa mema, Ewe Aongozaye kwenye haki iliyo wazi.