Baraza la Maimamu wa Jamaa wa Luxembourg limetangaza siku ya tarehe 1 Agosti kuwa ndiyo siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2011 Jul 18 , 17:58
Kongamano la Kimataifa la "Ustaarabu wa Kiislamu na Utambulisho wa Melayu" limepangwa kufanyika nchini Malaysia tarehe 14 na 15 Julai katika jimbo la Malacca nchini Malaysia.
2011 Jul 11 , 17:49
Nakala nadra sana ya Qur'ani iliyoandikwa katika zama za utawala wa Kiothmani itaonyeshwa katika Jumba la Makumbusho la Riyadh, Saudi Arabia.
2011 Jul 11 , 17:26
Maonyesho ya mchango wa Waislamu katika Uwanja wa Sayansi na Teknolojia yatafanyika tarehe 3 Septemba mwaka huu katika jimbo la California Marekani.
2011 Jul 02 , 20:24
Jumba la Makumbusho la Imam Hussein litafunguliwa siku chache zijazo katika sherehe zitakazofanyika kwenye mji mtakatifu wa Karbala.
2011 Jun 28 , 13:51
Baada ya kuchaguliwa imam bora wa swala ya jamaa kupitia kipindi kimoja cha televisheni nchini Malaysia, televisheni nyingine binafsi ya nchi hiyo ina mpango wa kuandaa kipindi kingine cha kuchagua mwanamke bora zaidi anayehubiri Uislamu nchini humo.
2011 Jun 26 , 16:25
Athari na kazi za kaligrafia ya Kiislamu zinaonyeshwa katika maonyesho ya kaligrafia yaliyopewa jina la Rana Riyadh Ahmad, mchoraji mashuhuri wa Pakistan. Maonyesho hayo yanaendelea katika Jumba la Kitaifa la Sanaa ya Pakistan huko katika mji mkuu Islamabad.
2011 Jun 22 , 14:38
Wizara ya Utamaduni ya serikali ya Hamas katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa maonyesho ya kwanza ya kimataifa yamepangwa kufanyika katika Ukanda huo kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Oktoba kwa ushirikiano wa wachapishaji na wasambazaji wa vitabu wa nchi za Kiarabu.
2011 Jun 22 , 14:33
Mtayarishaji mashuhuri wa filamu wa Iraq Jamal Amin al Hassani amesema kuwa anatayarisha mpango wa kufanya tamasha ya kimataifa ya filamu ya Uislamu na Imam Huusein (as) katika mji mtakatifu wa Karbala.
2011 Jun 20 , 19:26
Shughuli ya Ujue Uislamu imepangwa kufanyika tarehe 16 Julai katika kituo cha Kiislamu cha Britani (UKIM) katika mji wa Birmingham, Uingereza.
2011 Jun 20 , 19:25
Kongamano la saba la kila mwaka la vijana wa Ufaransa limepangwa kufanyika leo Jumapili tarehe 19 Juni katika jimbo la Bourgogne chini ya anwani ya 'Siku ya Masomo.'
2011 Jun 19 , 15:54
Leo ambapo Waislamu wanajitayarisha kusherehekea na kuadhimisha siku ya kuzaliwa Amirul Muuminin Imam Ali bin Abi Twalib (as), kundi kubwa la malenga limekutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusoma mashairi yao ambayo anglabu yalihusu masuala ya kidini, kimaadili na mwamko wa Kiislamu.
2011 Jun 17 , 15:24
Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali (as) katika mji wa Vienna nchini Austria, leo Jumatano kinaandaa sherehe maalumu ya kuadhimisha uzawa wa Imam huyo mtukufu wa Nyumba ya Mtume (saw).
2011 Jun 15 , 18:28