Kutokana na kuongezeka idadi ya watu wanaoomba kupata maarifa ya Kiislamu kwa upande mmoja na uhaba wa vituo vya kidini katika kujibu na kutosheleza maombi hayo kwa upande wa pili, taasisi ya kimataifa ya Jamiatul Mustafa (saw) imepanga kueneza shughuli zake na kuanzisha vyuo vikuu vya kidini na taasisi za Qur'ani katika nchi mbalimabli za dunia.
2010 Aug 25 , 11:19
Kongamano la wanakaligrafia bora zaidi wa Qur'ani katika nchi za Kiislamu litafanyika kuanzia tarehe 25 hadi 28 ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa lengo la kuandika kaligrafia ya msahafu kamili.
2010 Aug 24 , 12:39
Jumuiya ya wachapishaji vitabu vya watoto na vijana Iran imewasilisha zaidi ya anuani 800 za vitabu vya kidini na Qurani katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qurani ya Tehran.
2010 Aug 23 , 18:40
Ensaiklopidia ya Mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) iliyotayarishwa kwa lugha ya Kiingereza inaonyeshwa kwenye kitengo cha Athari za Taaluma ya Qur’ani za Ulimwengu wa Kiislamu katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur’ani yanayoendelea mjini Tehran.
2010 Aug 23 , 15:13
Ensaiklopidia ya Elimu na Wasomi wa Kiislamu iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza inaonyeshwa katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu mjini Tehran.
2010 Aug 22 , 00:37
Mkurugenzi wa jumba la makumbusho ya Kiislamu la Misri amesema kuwa maonyesho makubwa ya athari na turathi za kihistoria kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu yanafanyika katika jumba hilo la makumbusho.
2010 Aug 21 , 16:06
Maonyesho ya “Sanaa, Uislamu na Ulaya” yatafanyika kwa mwezi moja nchini Ufaransa kuanzia Septemba mosi katika Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu mjini Paris.
2010 Aug 21 , 15:17
Ensaiklopidia ya “Utamaduni na Ustaarabu wa Kiislamu” kwa lugha ya Kiingereza inauzwa katika kibanda cha ‘Athari za utafiti wa Qur'ani za Ulimwnegu wa Kiislamu’ katika Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran.
2010 Aug 19 , 11:41
Maonyesho ya Kimataifa ya “Uvumbuzi elfu moja na moja wa Kiislamu” yameanza Jumatano hii nchini Uturuki katika "Medani ya Sultan Ahmet’ mjini Istanbul.
2010 Aug 18 , 16:00
Athari za sanaa nadra za kale za Kiislamu zinaonyeshwa katika Kituo cha Kimataifa cha Masuala ya Fedha cha Dubai kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
2010 Aug 17 , 19:18
Kikao cha “Visa vya Qurani katika Zama Hizi” kitafanyika baadaye wiki hii huko Istanbul Uturuki chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Kiutamaduni na Utafiti ya Divander.
2010 Aug 15 , 12:55
Taasisi ya Kiutamaduni na Utafiti ya Imam Musa Sadr imewasilisha tafsiri ya Qurani ya Imam Musa Sadr katika Maonyesho ya 18 ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran.
2010 Aug 12 , 13:33
Maonyesho ya 18 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu yanayofanyika mjini Tehran yana kitengo maalumu cha vijana kinachotoa mafunzo mbalimbali ya Qur'ani Tukufu.
2010 Aug 10 , 07:42