Chuo cha Utamaduni na Sanaa cha Iran kimeandaa kikao cha kuchunguza athari za Mshairi ya Saadi kwa sanaa ya Kiirani na Kiislamu, kwa mnasaba wa kuadhimishwa siku ya kimataifa ya mshairi huyo mashuhuri.
2009 Apr 16 , 12:42
Kikao cha kimataifa cha Nafasi ya Elimu Katika Uislamu ambacho kimeandaliwa na Kituo cha Utamaduni wa Kiislamu cha Algeria kitafanyika leo Jumanne na kesho Jumatano huko Algiers, mji mkuu wa nchi hiyo.
2009 Apr 14 , 13:01
Uislamu na haki za binadamu umechunguzwa katika toleo jipya la jarida la Ujerumani la Fikra na Sanaa ambalo huchapishwa na Kituo cha Ujerumani cha Goethe.
2009 Apr 14 , 13:00
Filamu ya Maryam Mtakatifu iliyotengenezwa Iran imeanza kuonyeshwa katika televisheni ya taifa ya Zimbabwe.
2009 Apr 13 , 15:04
Filamu ya matukio ya kweli (documentary) ya Haki za Binadamu iliyotengenezwa nchini Iran ambayo inahusu manyanyaso yaliyofanywa na Wazayuni dhidi ya kuhani mmoja wa Kiyahudi imefainikiwa kuingia katika fainali ya tamasha ya filamu ya al Jazeera huko Doha, Qatar.
2009 Apr 13 , 15:01
Mchezo wa kuigiza wa "Mbwamwitu Nyumbani" umeanza kuonyeshwa nchini Syria katika harakati za kuwaunga mkono na kuwasaidia watoto wa Ukanda wa Gaza.
2009 Apr 12 , 14:34
Mkutano wa kimataifa wa Anthropolojia katika Utamaduni wa Kiislamu umeanza kazi zake katika mji wa Qayrawan nchini Tunisia.
2009 Apr 11 , 14:05
Kitabu cha Nahjul Balagha kinachokusanya hotuba, semi za hekima na barua za Imam Ali bin Abi Twalib (as) kimeanza kutarjumiwa na kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili.
2009 Apr 09 , 12:55
Farid Jauhar al-Kalam, mtarujumi na mwandishi mashuhuri wa vitabu, anaamini kwamba tarjumi nyingi za Qur'ani zinaoonyesha wazi kwamba watarjumi wengi wa kitabu hiki kitakatifu hawazingatii sana mahitaji ya wasomaji wao katika shughuli yao hiyo.
2009 Apr 08 , 12:07
Halmashauri ya Udugu wa Kiislamu ya Afghaistan kwa ushirikiano wa Baraza la Maulamaa wa Kishia na Kisuni la Mkoa wa Balkh imeamua kutuma ujumbe wa kutathmini vituo vya kielimu na kidini, misikiti pamoja na vituo vya masomo ya kidini katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Afghanistan.
2009 Apr 08 , 11:59
Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni wa Kiislamu la Umoja wa Nchi za Kiislamu Esesco, linashiriki katika kikao cha kimataifa kinachojadili urithi wa kiutamaduni wa Kiislamu mjini Amman Jordan.
2009 Apr 06 , 08:59
Mkusanyo wa mashairi ya 'Mimi na Quds Tukufu' ulioandikwa na Suleiman al-Aisi, mshairi mashuhuri wa Syria umechapishwa mjini Damascus, mji mkuu wa nchi hiyo.
2009 Apr 06 , 08:57
Kitabu cha 'Maisha ya Wasafi' kimechapishwa nchini Bulgaria kwa udhamini wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as).
2009 Apr 05 , 12:03