Kitabu cha 'Maisha ya Wasafi' kimechapishwa nchini Bulgaria kwa udhamini wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul Bait (as).
2009 Apr 05 , 12:03
Kitabu cha "Nabii wa Mwisho" kimezinduliwa katika sherehe iliyofanyika katika Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Islamabad, Pakistan.
2009 Apr 05 , 11:19
Filamu za kidini na Qur'ani zinatofautiana kidogo na filamu nyinginezo na kwa msingi huo mambo yanayotoa mvuto maalumu katika filamu hizo hayapaswi kupuuzwa. Hayo yamesemwa na Mehran Rajabi, mchezafilamu mashuhuri wa Iran.
2009 Mar 26 , 20:36
Sekta ya filamu ya Iran inaweza kuwa na ubora wa athari za Qur'ani iwapo tu wanaotengeneza filamu hizo watakuwa na ufahamu wa kutosha kuhusiana na kitabu hicho kitakatifu.
2009 Mar 18 , 14:37
Katika baadhi ya beti zake za mashairi, Maulana, mshairi mashuhuri wa Iran ambaye ana umaarufu mkubwa katika ngazi za kimataifa anasema kuwa majira ya machipuo ni ishara ya ufufuo katika siku ya Kiama na kufichuka kwa siri za wanadamu.
2009 Mar 18 , 14:33
Chuo Kikuu cha Princeton katika jimbo la New Jersey nchini Marekani kimezindua maktaba ya mtandao ambapo kimeweka humo karibu nuskha 200 za nyaraka za Kiislamu zilizoandikwa kwa mkono ili zipate kusomwa na watu.
2009 Mar 18 , 14:25
Kikao cha tano cha nuskha zilizoandikwa kwa mkono za Kiislamu kitafanyika tarehe 24 hadi 26 mwezi Agosti katika Chuo Kikuu cha Cambridge nchini Uingereza.
2009 Mar 12 , 14:03
Msanii wa Birjand katika mkoa wa Khorasan amekuwa akiandika maandiko madogo kwenye punje za mchele na ufuta. Kwa mujibu wa Iqna kutoka mkoani humo, msanii huyo Sayyid Majid amekuwa akiandika maandishi hayo yakiwemo ya aya za Qur'ani katika punje hizo ndogo, jambo ambalo limewavutia watu wengi.
2009 Mar 12 , 13:49
Tovuti ya Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha mjini Washington imechapisha jarida maalumu ambalo limepewa jina la Itra ya Mtume Muhammad (saw) kwa mnasaba huu wa kuzaliwa mtukufu huyo.
2009 Mar 11 , 09:58
Mkuu wa masuala ya habari na mawasiliano katika Haram ya Imam Ridha (as) huko katika mji mtakatifu wa Mash'had ametangaza ratiba ya sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (saw) na vilevile Wiki ya Umoja wa Kiislamu katika haramu hiyo.
2009 Mar 11 , 09:54
Muhammad Hussein Sufi, Naibu Mkuu wa Taasisi ya Idhaa na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB akiwa na wakuu wengine wa taasisi hiyo ameonana na kuzungumza na mamarja' pamoja na wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu katika mji mtakatifu wa Qum.
2009 Mar 11 , 09:49
Kitabu cha 'Utangulizi wa Usomaji Qur'ani' na maudhui ya 'Mwalimu wa Pili' chenye kurasa 128 na kilichoandikwa na Raminof kimechapishwa na taasisi ya Ilya nchini Russia.
2009 Mar 10 , 18:46
Kitivo cha Elimu ya Tiba na Huduma za Afya cha Chuo Kikuu cha Beheshti kimeandaa kikao cha kwanza cha kitaifa cha Utamaduni na Urithi wa Tiba ya Kiislamu na Iran.
2009 Mar 10 , 18:30