Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu imeanza katika mji wa Pretoria nchini Afrika Kusini ikisimamiwa na Kamati ya Utendaji ya Wiki ya Kiutamaduni na Kiislamu katika nchi mbalimbali za Kiislamu kwa kushirikiana na baraza la mji wa Pretoria.
2009 Feb 01 , 11:30
Kitabu cha "Demokrasia ya Kidini, Hakika, Maana na Maswali ya Kisiasa" kimechapishwa katika mji wa Saint Petersburg nchini Russia.
2009 Feb 01 , 11:12
Maonyesho ya kimataifa ya Mfungamano na Watoto wa Ukanda wa Gaza yamenza mjini Muscat, Oman.
2009 Feb 01 , 11:11
Maonyesho ya sanaa ya uchoraji yaliyopewa jina la "Bosnia Jana, Leo Gaza" yamefunguliwa katika mji wa Sarajevo huko Bosnia Herzegovina kwa shabaha ya kuonyesha jinai zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
2009 Jan 31 , 11:08
Jumuiya ya Fiqhi ya Qur'ani na Sunna za Mtume (saw) ya Misri imejishindia tuzo ya kimataifa ya Mfalme Faisal wa Saudi Arabia ya mwaka huu wa 2009 kutokana na huduma zake kwa Uislamu.
2009 Jan 29 , 11:57
Waziri Mkuu wa Hungary Ferentsem Dyurchanem ametembelea jengo la makumbusho la Sanaa za Kiisalmu nchini Qatar na kusema athari za sanaa zilizopo katika jumba hilo ni dhihirisho la kunawiri ustaarabu na utamaduni wa Kiislamu katika zama tofauti.
2009 Jan 27 , 15:26
Kikao cha tatu cha kuwaenzi wachapishaji na wahifadhi bora zaidi wa Qur'ani Tukufu kitafanyika hivi karibuni katika mwaka wa 30 wa kuadhimishwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
2009 Jan 27 , 14:13
Mashindano ya kiutamaduni kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran yanatazamiwa kufanyika nchini China kwa udhamini wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini humo. Mashindano hayo yanafanyika kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 30 tangu baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.
2009 Jan 27 , 13:45
Mkutano wa Uislamu na Ubuddha unatazamiwa kufanyika tarehe 6 Februari katika Chuo Kikuu cha Mahachulalongkomrajavidyalata nchini Thailand. Mkutano huo utasimamia na chuo hicho na Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Thailand.
2009 Jan 27 , 13:42
Mashindano ya kwanza ya kimataifa ya uchoraji kwenye kuta kwa ajili ya kurembesha kuta za mji mtakatifu wa Makka yameanza kwa kuhudhuriwa na Usama bin Fadhl al-Bar, Meya wa mji huo.
2009 Jan 26 , 13:46
Waandishi wa weblogu nchini Iran wamemundikia barua Waziri wa Elimu wakitaka vitabu kuhusu mapambano ya watu wa Gaza viongezwe katika mitaala mashuleni.
2009 Jan 24 , 16:14
Maonyesho ya picha yanayojadili jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza yamefanyika nchini Uturuki kwa udhamini na usimamizi wa Mursalin Tan, mwandishi mashuhuri wa nchi hiyo, katika mji wa Istanbul.
2009 Jan 24 , 08:37
Maonyesho ya 'Palestina na mapambano katika kioo cha Sanaa' yamefunguliwa mjini Damascus Syria kwa udhamini wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
2009 Jan 24 , 08:06