IQNA

Ushauri kwa watu wenye kisukari katika Saumu ya Ramadhani

17:11 - May 30, 2016
Habari ID: 3470346
Siku chache zimesalia kabla ya kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na Waislamu wanajitayarisha kuukaribisha mwezi huo na kutekeleza ibada ya Saumu au kufunga.

Kwa Waislamu wote ni mwezi wa ibada na kufunga kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa katika mafundisho ya Kiislamu. Hatahivyo, kwa wale wenye ungonjwa wa kisukkari au diabetes, huwa vigumu kuweza kutekeleza ibada ya funga na wakati huo huo kuhakikisha kuwa hakuna madhara katika kiwango cha sukari mwilini.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Jumapili iliyopita kumefanyika kikao nchini Canada cha kutoa ushauri kwa watu wenye ugonjwa wa sukari wajumuike na Waislamu wengine katika kufunga Sawm ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Daktari Tyceer Abouhassan na mtaalamu wa lishe Nouhad Mokdad wameshiriki katika kikao cha kutao ushauri na kusisitiza kuhusu nukta tano zifuatazo.

Vyakula vya Carbohydrate au wanga na Protini

Bi. Mokdad anasema ni muhimu kuhakikisha chakula unachokula kina protini na carbohydrate au wanga ili kiwango cha sukari mwilini kibakie kuwa wastani siku nzima. Aidha ansisitiza kuhusu kujiepusha kutumia vinyaji vyenye sukali kama saoda na juice.

Baadhi ya vyakula vilivyo na wanga ni: viazi, vyakula vya nafaka (mchele, mahindi, mtama) na vinginevyo. Vyakula vyenye protini ni kama samaki, nyama, maharage na mayai. Protini pia hupatikana kwenye matunda na mboga mboga.

Fungua sawmu kwa mlo mdogo

Bi. Mokdad anashauri kuwa, badala ya kufungua saumu na mlo mkubwa, mwenye kufunga anapaswa kuanza na mlo mdogo kama vile tende na maji na kisha baada ya kupumzika aanza kula saladi na kishe vyakula vyenye protini au nafaka. Anasema kula chakula kwa utaratibu huo humsaidia mwenye kufunga kujizuia kula kupita kiasi na pia husaidia viritubisho kuingia na kutulia mwilini.

Kunywa maji mengi

Daktari Abouhassan anasharui kunywa kwa wastani glasi nne za maji baina ya wakati wa kufuturu na daki. Hii ni kwa sababu maji iwapo mwili una maji ya kutosha basi mwenye Saumu hujiepusha na baadhi ya matatizo kama vile maumivi kichwani.

Mazooezi ya kimwili

Mazoezi husaidia mwili kuratibu ipasavyo kiwango cha sukari. Hatahivyo unapaswa kuchukua tahadhari wakati wa mazoezi hasa iwapo kuna joto kali. Halikadhalika unapaswa kupima kiwano cha sukari mara kwa mara siku nzima. Inapendekezwa kuwa mwenye kufunga apimwe kiwango cha sukari kila wakati anaposwali.

Daktari Abouhassan na Mokdad wanasisitiza kuwa, pamoja na kuwa saumu ni sehemu muhimu ya ibada za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini suala la afya na uwezo wa mwenye kufunga pia limepewa uzito mkubwa na Uislamu. Kwa msingi huo watu wenye maradhi, ambayo huzorotesha afya iwapo mtu atakuwa katika Saumu, kama vile kisukari, wanashauriwa kuwasiliana na daktari mwenye kuaminika ili kubaini iwapo Saumu itakuwa na madhara au la.



3459954
Kishikizo: saumu ramadhani iqna
captcha