IQNA

Watetezi wa Qur'ani

Kiongozi wa Hizbullah: Lazima kilipizwe kisasi kwa jasusi wa MOSSAD aliyeichoma moto Qur'ani Tukufu

21:07 - August 02, 2023
Habari ID: 3477370
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amewataka vijana wote wa Kiislamu wasisubiri kauli za jumuiya na mashirika bali wachukue hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya mtu aliyeichoma moto Qur'ani.
Mnamo tarehe 28 Juni, na huku akipewa ulinzi na Polisi ya Sweden, mkimbizi wa Kiiraqi Salwan Momika aliichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu mbele ya msikiti wa Stockholm. Kwa mara ya pili aliukanyaga kanyaga Msahafu mbele ya ubalozi wa Iraq mjini Stockholm na kupiga kelele za matusi dhidi ya Uislamu.
 
Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah, amesema katika hotuba aliyotoa katika mji wa Al Nabatiya ulioko kusini mwa Lebanon kwa mnasaba wa mwezi 13 Muharram kwamba kuichoma moto Quran Tukufu ni changamoto ya kuwatusi Waislamu bilioni mbili duniani.
Nasrullah amefafanua kwa kusema: "haingepasa mtu huyu ambaye ni jasusi wa Mossad awatusi Waislamu, na suala hili linaonyesha usaliti na unafiki wa Sweden na nchi za Magharibi kwa ujumla".

Katibu Mkuu wa Hizbullah amelaani kimya cha baadhi ya nchi za eneo na dunia kuhusiana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu na akasema, katika baadhi ya nchi, kama angevunjiwa heshima Mfalme, Mwanamfalme au familia yake, dunia ingesimama wima na wala isingenyamaza kimya, bali mahusiano pia yangevunjwa.

 
Sayyid Hassan Nasrullah amesema kama Lebanon ingezisubiri Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, nchi hii pia ingeenda na maji, lakini Lebanon iliwaamini marafiki zake wachache hususan Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Syria na haikuruhusu nchi hii ivamiwe na kukaliwa kwa mabavu.
 
Nasrullah ameongezea kwa kusema: "Sweden na Denmark si nchi za kutushughulisha na kuzipa uzito. Tuko katika zama za ushindi na tunawaambia wananchi wa Palestina wasiwategemee kwa namna yoyote ile watawala wa Kiarabu, bali wategemee nguvu na juhudi za vijana wao.
 
Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, hii leo mhimili wa Muqawama wa Iraq, Iran na Lebanon hautawaruhusu Wazayuni waiangamize Palestina.

3484605

Habari zinazohusiana
captcha