IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Afisa wa zamani wa UN: Hakuna chochote kinachoweza kuhalalisa kuchomwa kwa Vitabu Vitakatifu

16:20 - August 08, 2023
Habari ID: 3477401
WASHINGTON, DC (IQNA) - Mwandishi maalum wa zamani wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kwamba hakuna lengo halali kwa kuruhusu vikundi kuchoma vitabu vitakatifu.

Richard Falk, profesa mstaafu wa sheria za kimataifa katika Chuo Kikuu cha Princeton alisema wimbi la hivi majuzi la uchomaji Qur'ani Tukufu nchini Uswidi na Denmark ni "mpango mpana wa kuwapinga wahamiaji na wasiokuwa wa Ulaya ambao umekua wa kisiasa kikamilifu."

"Hakuna lengo halali kwa kuruhusu vikundi kuchoma maandiko matakatifu ya imani nyingine ya kidini," aliongeza.

"Kwa mtazamo wangu vitendo hama hivi havifai na vinapaswa kupigwa marufuku."

Katika miezi ya hivi karibuni makundi ya misimamo mikali ya mrengo wa kulia yamevunjia heshima na kuchoma nakala kadhaa za Qur'ani nchini Denmark na nchi jirani ya Uswidi, jambo ambalo limekuwa likilaaniwa vikali na Waislamu kote duniani na kutaka kuchukuliwa hatua za kukomesha vitendo hivyo.

Profesa Falk amesema inawezekana kupiga marufuku vitendo vya kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu chini ya katazo la matamshi ya chuki, ambalo lipo katika nchi kama Uingereza na Ujerumani, kwa mfano," na hivyo sheria kama hiyo inaweza kutumika katika nchi za Skandinavia.

Falk alisema nchi hizi zinaweza kupitisha sheria za kuzuia mashambulizi dhidi ya vitabu vitakatifu, akisisitiza kwamba "zitakuwa na uungwaji mkono mkubwa wa kimataifa katika hatua hii."

"Kwa sababu kuna azimio la hivi karibuni la Umoja wa Mataifa ... ambalo linasema ni kinyume na sheria za kimataifa, kuchoma au kuharibu vinginevyo," alisema.

Hata hivyo amebainisha kuwa, azimio la hivi karibuni la Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa lililolaani vitendo vya chuki za kidini, ikiwemo mashambulizi dhidi ya Qur'ani, lilipingwa na nchi 12 zikiwemo madola ya Magharibi kama Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.

Waislamu kote ulimwenguni wana wasiwasi kuwa mashambulizi haya yanayoongezeka dhidi ya Quran yanaweza kusababisha ghasia zaidi dhidi ya jamii yenyewe.

Huku uchomaji vitabu umekuwa mojawapo ya kampeni kuu za Wanazi katika kuelekea Mauaji ya Kimbari, Falk alionya kuwa "jamii za kidemokrasia zinapaswa kuwa macho dhidi ya kurudiwa kwa aina hii ya tabia ya mauaji ya kimbari, kwa sababu ni wazi inaweza kurudiwa."

"Kwa kiasi fulani, imerudiwa hivi majuzi nchini Myanmar, ambapo Waislamu wachache ... walikabiliwa na kile ambacho waangalizi wengi wamekielezea kama mauaji ya halaiki," alisema, akimaanisha hali mbaya ya jamii ya Rohingya.

Falk, ambaye alihudumu katika tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina na pia mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu katika maeneo ya Palestina, aliongeza kuwa watu wa Palestina pia kwa muda mrefu wamebaguliwa kimfumo kiasi kwamba hali yao imefasiriwa kama ubaguzi wa rangi ... na wengine wamedai kuwa ni sawa na tabia ya mauaji ya kimbari."

Huu ni wakati wa kuwa macho kuhusu kuruhusu ishara kama hizo za uhasama, alisema.

3484684

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watetezi wa qurani
captcha