IQNA

Watetezi wa Qur'ani Tukufu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa: Viongozi wa Kiislamu walaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

22:30 - September 20, 2023
Habari ID: 3477627
NEW YORK (IQNA) - Viongozi kadhaa wa nchi Kiislamu duniani wamehutubu kwenye Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo wamelaani vikali kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu.

Akihutubia kwenye hafla hiyo mjini New York siku ya Jumanne, Rais wa Iran Ebrahim Raeisi aliitaja Qur'an Tukufu kama "kitabu kinachomwalika mwanadamu kwenye busara, masuala ya kiroho, uadilifu, maadili na ukweli," ambacho kinategemea nguzo tatu za "tauhidi, uadilifu na utu wa mwanadamu. ”

“Rais wa Iran ameyanyua juu Qur'an Tukufu na kuwapa ujumbe walimwengu kwa kusema: "Qur'an hii ni yenye mafunzo adhimu sana, ni Kitabu kinachotengeneza utamaduni mzuri wa Mwanadamu, ni Kitabu Kitukufu kinachomtengeneza vyema Mwanadamu, ni kitabu chenye kutengeneza jamii ya mwanadamu, ni kitabu cha milele, na kuupotosha ukweli wa Qur'an ni kitu ambacho hakiwezekani, hii Qur'an huwezi kuichoma moto na kuipoteza abadan"...

Akilaani vitendo vya karibuni vya kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi za Uswidi na Denmark Rais wa Iran amesisitiza kuwa, "Tunaamini kuwa, kuheshimiwa matukufu ya kidini kunapasa kuwa moja ya ajenda kuu za Umoja wa Mataifa."

 Aidha amebaini kuwa Qur'an Tukufu inakataza mawazo na imani za matusi, na inawaheshimi Manabii Ibrahim, Musa, na Isa kama heshima kwa Muhammad (SAW)," Raisi alisema na kuongeza, "Dhana hizi zinazounganisha na manabii watukufu, wenye kutia moyo, wa ubinadamu, wa kujenga jamii na kujenga ustaarabu. kwa kuwa jamii za wanadamu ni za milele na hazitaungua. Moto wa matusi na upotoshaji hautakuwa mpinzani wa ukweli kamwe."

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan - ambaye ameweka shinikizo kwa miezi kadhaa kwa Uswidi kutokana na sera nchi hiyo ya Ulaya za kurhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu amesema kuwa nchi za magharibi zinakabiliwa na "tauni" ya ubaguzi, ikiwa ni pamoja na chuki dhidi ya Uislamu.

"Imefikia viwango visivyovumilika," aliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

"Mtazamo unaohimiza mashambulizi ya kutisha dhidi ya Qur'ani Tukufu huko Ulaya, kwa kuwaruhusu chini ya kivuli cha uhuru wa kujieleza, kimsingi unatia giza mustakabali wa [Ulaya] kupitia mikono yake yenyewe."

Amir wa Qatar, Sheikh Tamim, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alisema kuwa "kuhatarisha utakatifu wa wengine kwa makusudi" haipaswi kuonekana kama uhuru wa kujieleza.

"Ningewaambia ndugu zangu Waislamu kwamba haiwezekani kwetu kukengeushwa na mjinga au mtu wakati wowote anapoamua kutuudhi kwa kuchoma Qur'ani Tukufu au kwa aina zingine za upuuzi," Sheikh Tamim alisema.

"Qur'an ni takatifu sana haiwezi kuathiriwa na vitendo viovu vya kuivunjia heshima mtu asiye na akili."

3485243

Habari zinazohusiana
Kishikizo: watetezi wa qurani
captcha