IQNA

Waislamu nchini Marekani wanabaguliwa sana

22:14 - February 25, 2015
Habari ID: 2897132
Waislamu nchini Marekani wameelezea wasi wasi wao kutokana na kuongezeka wimbi la ubaguzi na hujuma dhidi yao.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Yougav, asilimia 73 ya watu walioshiriki wa uchunguzi huo wa maoni walithibitisha kwamba, mbali na wasi wasi iliyo nayo jamii hiyo ya Waislamu, lakini pia wanakabiliwa na wasiwasi mkubwa wa mashambulizi ya kibaguzi dhidi yao nchini Marekani. Aidha asilimia 63 ya washiriki wa uchunguzi huo wa maoni wamesema kuwa, baada ya Waislamu, wahanga wa pili wa mashambulizi hayo ya kibaguzi nchini humo ni Wamarekani wenye asili ya Kiafrika. Hii ni katika hali ambayo asilimia 60 nyingine ya Wamarekani wanaokabiliwa hujuma hizo za kibaguzi ni Wamarekani wenye asili ya Mexico ambao wanashika nafasi ya tatu kwa kubaguliwa. Suala la ubaguzi limekuwa kwa muda mrefu tatizo sugu ambapo kwa mara kadhaa kumekuwa kukishuhudiwa vitendo vya ubaguzi hususan dhidi ya raia wa nchi hiyo wenye asili ya Afrika. Ubaguzi dhidi ya jamii ya watu hao unarejea nyuma hadi katika kipindi cha biashara ya utumwa katika karne ya 17 Miladia ambapo mamilioni ya watu walipoteza maisha yao katika biashara hiyo haramu....mh

2894818

captcha