IQNA – Kwa mujibu wa mtazamo wa Kiislamu, binadamu wote ni waja wa Mwenyezi Mungu, na mali yote ni ya Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, mahitaji ya wale wasiojiweza yanapaswa kutimizwa kupitia ushirikiano wa kijamii.
IQNA – Usajili umefunguliwa rasmi kwa toleo la 21 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu nchini Algeria, mojawapo ya mashindano yenye heshima kubwa katika kanda ya Afrika Kaskazini.
IQNA – Maktaba mbalimbali nchini Tunisia, zikiwemo zile za vyuo vikuu vya Zaytouna na Kairouan pamoja na maktaba binafsi, zimehifadhi maelfu ya maandishi ya kale yaliyojumuishwa kutokana na karne nyingi za juhudi za kielimu.
IQNA – Washiriki wa kitengo cha wanawake katika Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran waliendelea kuonesha umahiri wao siku ya tatu ya mashindano hayo, wakishindania nafasi za juu.
IQNA – Polisi nchini New Zealand wanafanya uchunguzi kuhusu tishio la bomu lililolenga Msikiti wa Kilbirnie uliopo Wellington, hali iliyosababisha kusitishwa kwa shughuli zote za msikiti huo kwa muda.
IQNA – Kwa kuboresha mazingira ya upangaji na uamuzi, na kuongeza ushiriki wa washiriki wenye hamasa, mashindano ya kuhifadhi Qur’ani ya Australia yamegeuka kuwa mfano bora wa kuimarisha utambulisho wa vijana Waislamu nchini humo.
IQNA – Waziri wa Mambo ya Waqf wa Misri ametoa pongezi zake kwa kuenziwa hivi karibuni kwa Qari maarufu Sheikh Abdul Fattah Taruti wakati wa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani yaliyofanyika mjini Moscow, Russia
IQNA – Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amemtaja Allamah Mirza Muhammad Hussain Naeini (Rehmatullah alayh) kama mmoja wa nguzo mashuhuri zaidi za kielimu na kiroho katika Hawza (Chuo kikuu cha Kiislamu) ya kale ya Najaf, Iraq.
IQNA – Mamlaka za Palestina zimeonya kuwa shughuli za uchimbaji zinazofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel karibu na Msikiti wa Al-Aqsa na katika Mji wa Kale wa Al-Quds (Jerusalem) zinaweza kuhatarisha uimara wa msikiti huo mtukufu.
IQNA – Mwanazuoni mwenye msimamo wa kihafidhina na aliye katika miaka ya tisini ameteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa kidini au Mufti Mkuu nchini Saudi Arabia, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
IQNA – Serikali ya Ufilipino imezindua mpango mpya wa kukuza nafasi ya taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Asia katika soko la kimataifa la utalii 'Halal', linalokua kwa kasi.
IQNA – Katika tukio la kihistoria lililopeperushwa kupitia kipindi cha televisheni cha Ahl Masr nchini Misri, tafsiri ya Qur'ani Tukufu iliyoandikwa kwa mkono na mwanazuoni mashuhuri wa Al-Azhar, marehemu Sheikh Ahmed Omar Hashem, imewasilishwa kwa mara ya kwanza hadharani. Kazi hiyo ya miaka kumi imekamilika kabla ya kifo chake mapema mwezi huu.
IQNA – Mtandao wa Mazungumzo ya Kiislamu nchini Norway (Islamic Dialogue Network) umezindua tovuti ya kwanza ya kitaifa ya kupambana na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia), iitwayo stoppmuslimhat.no.
IQNA- Kufuatia ongezeko kubwa la uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu nchini Uingereza, serikali inatarajiwa kutangaza ufafanuzi mpya wa neno “'Chuki Dhidi ya Uislamu' (Islamophobia)”—ambapo huenda likabadilishwa na kuwa “chuki dhidi ya Waislamu.”