IQNA

Saudia yaanza kuwazika kwa umati mahujaji waliopoteza maisha katika maafa ya Mina

20:07 - September 29, 2015
Habari ID: 3374469
Saudi Arabia imesema kuwa itawazika kwenye makaburi ya umati mahujaji walioaga dunia katika tukio la Mina ambao imeshindakana kutambuliwa.

Viongozi wa Saudia wamewaomba viongozi wa misafara mbalimbali ya Kiislamu nchini humo kushiriki kwenye shughuli ya kuwazika mahujaji wengi walioaga dunia huko Mina Alhamisi iliyopita, ambao wameshindwa kutambuliwa na jamaa zao, ambao idadi yao kwa uchache ni watu mia sita. Imearifiwa kuwa  miili ya mahujaji walioaga dunia imeharibika na kuna wasiwasi juu ya uwezekano wa kutokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu. Aidha upigaji picha mahujaji waliokufa umepigwa marufuku na kwamba viwiliwili vya wahanga hao vinatazamiwa kuzikwa katika makaburi ya umati. Utawala wa Aal Saud umechukua hatua hiyo huku misafara mingi ya nchi za Kiislamu ikibanisha wasiwasi wao baada ya kutoweka idadi kubwa ya mahujaji wao kwenye maafa ya Mina.../mh

3374142

Kishikizo: mina maafa umati makaburi
captcha