IQNA

Barua ya Kiongozi, Msingi wa Kuamiliana nchi za Kiislamu na Magharibi

22:45 - December 06, 2015
Habari ID: 3460507
Ali Larijani, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kwa vijana wa Magharibi ni msingi mpya wa kuamiliana ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi ambao umejengeka juu ya msingi wa mantiki, ukweli wa mambo na kuheshimiwa tamaduni.

Ameongeza barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kwa vijana wa Magharibi ni msingi mpya wa kuamiliana ulimwengu wa Kiislamu na Magharibi ambao umejengeka juu ya msingi wa mantiki, ukweli wa mambo na kuheshimiwa tamaduni.
Akizungumza leo Jumapili mwanzoni wa kikao cha Bunge, Spika Larijani amesema kuwa barua hiyo ya kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Magharibi imefunua pazia la unafiki mamboleo kwenye nyuso za usitikbari wa madola makubwa ya dunia na kuweka wazi sehemu kubwa ya ukweli wa mambo. Amesema, ulimwengu wa Kiislamu daima umekuwa ukipigana vita dhidi ya utumiaji mabavu wa kijahili na taasubi sizizo na msingi. Amesisitiza kuwa ugaidi katika Mashaiki ya Kati unaenezwa na njama za vibaraka na madikteta wanaotawala katika nchi za eneo hili kwa ushirikiano wa mashirika ya ujasusi ya madola makuu. Spika wa Bunge la Iran ameashiria ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kusema kuwa mapambano dhidi ya ugaidi huo hayahitajii majeshi ambayo kwa kawaida hufuatilia malengo mengine bali ni majeshi hayo yenyewe ndio yanayochochea ugaidi huo.
Larijani amesema amesema uingilijia wa kijeshi wa Uturuki huki Iraq ni tatizo jingine jipya ambalo limezushwa katika eneo kwa madhumuni ya kuimarisha ugaidi. Amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unafuatilia utulivu na usalama katika eneo na kuziomba nchi zote za eneo kushirikiana kwa nia njema kwa madhumuni ya kupambana na ugaidi.
Larijani pia ameashiria faili la nyuklia la Iran na kuashiria matumaini yake kuwa Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) italifunga kabisa faili bandia la tuhuma dhidi ya teknolojia ya nyuklia amani ya Iran na hivyo kuandaa uwanja wa kufikiwa mkataba wa mwisho wa nyuklia kati ya pande mbili.

Bonyeza hapa kusoma barua ya Kiongozi Muadhamu kwa Vijana wa Magharibi

3460155

captcha