Hayo yameelezwa na Ibrahim Hooper Mkurugenzi wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani ambaye amebainisha kwamba, Waislamu wanaoishi Marekani wanalalamikia gharama kubwa za mazishi na hatua ya viongozi wa nchi hiyo ya kutotoa ushirikiano kwa ajili ya kuzikwa Waislamu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu.
Inaelezwa kuwa, kwa kiwango cha wastani gharama za mazishi ya Mwislamu hugharimu kiasi cha dola elfu tano nchini Marekani. Mkurugenzi wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani amesema kuwa, tangu mwaka 2011 Waislamu wamekuwa wakitaka watengewe na serikali makaburi maalumu ya Waislamu mjini New York ili Waislamu wa mji huo wasilazimike kuwazika maiti wao katika jimbo la New Jersey, lakini hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na serikali kutekeleza ombi hilo.
Kwa mujibu wa Baraza la Mahusiano ya Kiislamu la Marekani ni kuwa,
Waislamu hugharamika mno katika suala la mazishi hasa gharama za usafiri
kutokana na kulazimika kusafirisha maiti wao masafa ya mbali kwa ajili
ya kwenda kuzika kutokana na kuwa maeneo wanayoishi hakuna makaburi ya
Waislamu.