Kwa mujibu wa taarifa, Sayyed Ali Abul-Hassan, Mkuu wa Darul Qur’an tawi la Lebanon amesema mafunzo hayo ya Qur’ani Tukufu yaliwalenga mamia ya wavulana na washichana katika msimu wa joto mwaka huu.
Ameongeza kuwa washiriki kutoka makundi mbali mbali ya umri walishiriki kutoka miji mikubwa na midogo zaidi ya 15.
Kozi hiyo ilijumuisha kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu na pia mashindano ya Qur’ani yaliyopewa jina la Al Ghadira. Washiriki bora walipata zawadi za fedha taslimu katika sherehe ya kuhitimisha kozi hiyo.