IQNA

Indhari ya Sheikh Sabri kuhusu njama ya Wazyuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa

11:19 - October 11, 2020
Habari ID: 3473249
TEHRAN (IQNA)- Sheikh Ekrima Sa'id Sabri, Mkuu wa Baraza Kuu la Kiislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) na khatibu katika Msikiti wa Al Aqsa mjini humo ametahadharisha kuhusu njama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kutaka kutwaa sehemu ya msikiti huo ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu.

Kwa mujibu wa tovuti ya paltoday.tv, Sheikh Sabri amesema utawala wa Kizayuni wa Israel hauheshimu hata kidogo Msikiti wa Al Aqsa. Ameongeza kuwa Israel inafanya juu chini kuhakikisha kuwa inakata mfungamano wa Waislamu na Msikiti wa Al Aqsa.

Aidha amesema utawala bandia wa Israel unaendelea kuwashajiisha Wazayuni wahamia Palestina kwa kuwaahidi kuwa msikiti wa Al Aqsa utabomolewa na mahala pake kujengwa hekali. Sheikh Sabri amesema utawala wa Israel unawahadaa walowezi wa Kizayuni kuwa ardhi ya Palestina ni ya Mayahudi na wana haki ya kuishi hapo.

Khatibu wa Msikiti wa Al Aqsa amesema tamaa ya Wazayuni maghaisbu haina kikomo na kwamba kila siku wanatekeleza njama dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa. Aidha amesema katika kipindi cha wiki tatu sasa Wazayui wamekuwa wakiwazuia Wapalestina kuingia Al Aqsa kwa kisigizio cha corona na hivyo wanapata fursa ya kutekeleza njama yao ya kuyahudisha eneo hilo takatifu la Kiislamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

3928517

captcha