Kwa mujibu wa taarifa, Msahafu huo ulitayarishwa na wanafunzi mwaka 2001 na umeweza kuwavutia wengi katika Kituo cha Kiislamu cha Jakarta.
Msahafu huo una urefu wa mita moja na upana wa sentimeta 50 na ulitayarishwa na wanafunzi Chuo Kikuu cha Sayansi za Qur’ani katika eneo la Java ya Kati.
Katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Waislamu kote duniani hujikurubisha zaidi na Qur’ani tukufu na kwa msingi huo mbali na kusoma pia hufanyika maonyesho ya Qur’anin katika nchi mbali mbali.